Habari za Punde

Uchaguzi wa Rais wa Chuo cha maendeleo na utalii Zanzibar

Na Miza Othmani Maelezo Zanzibar 6/4/2013 .
TUME ya Chuo cha maendeleo na utalii Zanzibar kimemtangaza rasmi mwanafunzi Mussa Mohd Rashid kuwa Rais wa chuo hicho .
Tume hiyo imetangaza Rais Mussa Moh’d baada ya uchaguzi uliyofanyika Maruhubi mjini Zanzibar
Katika kinyanganyiro cha Uchaguzi huo waligombania ni Juma Ali Abdalla na Mussa Moh’d Rashid waliopiga kura ni jumla wanafunzi 200 kura zilizoharibika 02, kura halali zilizopigwa ni 198, kwa upande wa matokeo, Juma Ali Abdalla amepata kura 97- 48.5% na mgombea mweza Mussa Moh’d Rashid alipata kura 101 -50%.
Hata hivyo kwa upande wa Rais Mussa Moh’d alisema kuwa kudumisha umoja na mashirikiano kutaondosha kugawanyika makundi na matabaka na kutaleta maendeleo chuoni hapo .

Aidha alisema kuwa katika madaraka aliyopewa atatekeleza ahadi zote alizoahidi na kuifanya serikali kuwa imara na yenye nguvu na kuepukana na migogoro ambayo yatakwamisha utekelezaji wa kazi.
“kuondoa makundi na kuondoa matabaka nitatekeleza ahadi zote nilizoahidi ”,Alisema Rais .
Alisisitiza kuwa wanafunzi atakuwa pamoja nao bega kwa bega katika matatizo mbali mbali yatakayojitokeza na kuwa imara katika kukabiliana na majukumu ya chuoni hapo .
Nae Omar Moh’d Khamis kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema kuwa kudumisha mashirikiano ya pamoja na uongozi wa chuo ndio njia pekee ya kuleta maendeleo na ufanisi mkubwa .
“tujenge mashirikiaano tuepukane na ubaguzi na kuleta maendeleo endelevu chuoni”Alisema Omar.
Uchaguzi huwo umefanyika baada ya Rais aliyokuwepo Bakar Haji Kheir kumaliza muda wake wa uongozi .

1 comment:

  1. Hebu twekee picha za Taa za Solar Energy zilizowekwa... Kwasababu naona hao Wapachikaji kama hawana utaalamu wakutosha...? Au ?.. Tuombe dua zisijeanguka..

    Wameweka Taa Unguja Pemba Mitaa na miji iko Gizani .. Serikali ya Mapinduzi ni Baguzi kama nini na kwasababu inaongozwa na Wamimi...

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.