Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa, Ndugu Martine Shigela akiwa anazungumza na kusisitiza jambo katika mkutano huo ambapo alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Donge wanayo bahati ya kuwa na mbunge anayewajali na kusaidiana nao katika kulijenga na kuliletea maendeleo jimbo la Donge.
Katibu wa Kikundi cha Ujasiriamali cha mkorofi si mwenzetu akipokea mchango wa shilingi 300,000 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM ndugu Sadifah Juma.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) na mbunge wa jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifah Juma, amefanya
mkutano wa hadhara jimboni humo ambapo amechangia takribani shilingi milioni 4,
ikiwemo pesa taslimu shilingi milioni tatu na laki mbili (3,200,000) pamoja na
vifaa vya ushoni vyenye thamani ya shilingi milioni 1 kwa vikundi mbalimbali
vya ujasiriamali vya jimboni Donge.
Sadifah amechangia kiasi hicho kwa vikundi 12 vya
ujasiriamali ambapo vikundi 4 vya ufugaji wa kuku wa kisasa vilipatiwa kiasi
cha shilingi laki 300,000 kila kimoja,vikundi hivyo ni Inshaallah Hatuchoki,
Letu moja , Sisi kwa sisi na kikundi cha Mkorofi si mwenzetu. Mbali na vikundi
hivyo pia vikundi vya utengenezaji matofali, vikundi vya ushonaji na vikundi
vya kukopeshana vilinufaika na michango ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Sadifah.
Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na viongozi
waandamizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka
Makao Makuu ya Jumuiya hiyo wa afisi kuu ya Zanzibar na Dar es salaam
wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ndugu Shigela Martine, Makatibu wa
Idara za Jumuiya hiyo na maafisa wa Makao Makuu, Mheshimiwa Sadifah ameichangia
timu ya mpira wa miguu ya Kata ya Vijibweni-mahonda vifaa vya michezo.
Mbali na michango hiyo ya fedha taslimu na nyenzo za
kimaendeleo, Mhe. Sadifah amesisitiza vijana wa jimbo hilo kujituma kwa hali na
mali katika kujiletea maendeleo binafsi na pia kushiriki katika shughuli za
utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo, akasisitiza kuthamini na
kuvitunza vifaa vlivyotolewa katika vikundi hivyo na kuvitumia ipasavyo ili
viweze kuwa msaada endelevu kwa vikundi hivyo.
Nae, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Martine Shigela
aliwasisitiza Vijana kuwa msitari wa mbele katika kushiriki shughuli mbalimbali
za mendeleo na kuwa mfano bora wa kufanikisha na kutekeleza Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi, lakini pia akawaahidi Vijana wa jimbo hilo kuwa Jumuiya ya Vijana
itawasaidia katika kuwapa mafunzo ya ujasiriamali ambayo Jumuiya hiyo inayatoa
kwa vijana mbalimbali hapa nchini ili kuwawezesha kushiriki shughuli za
kimaendeleo na ujasiriamali kwa uhakika na ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Sadifah yupo jimboni humo katika ziara mbalimbali
za kumuenzi muasisi wa Mapinduzi-Marehemu Abeid Aman Karume, aliyefariki tarehe
06th April 1972, ambapo kilele cha maazimisho ya kumbukumbu hizo
yatafanyika katika afisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo kisiwandui mjini
unguja kesho Jumapili tarehe 07th April 2013.
No comments:
Post a Comment