Habari za Punde

Kamera ya Martin Kabemba

  Wakulima wa mwani wameiomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Makampuni yanayonunua mwani kuwaongezea bei kutokana na gharama kubwa ya kilimo hicho kwa hivi sasa.
Pichani akina mama wa kijiji cha Kiwengwa Zanzibar wakichambua mwani baada ya kuvuna kondeni kama walivyokutwa na mpiga picha Martin Kabemba jana.
 Mzee Omar Makame ( 73 ) kutoka kijiji cha Kiwengwa mkoa wa Kaskazini Unguja akisuka makuti kwa ajili ya kuuza ambapo anaelezea kuwa kazi hiyo inampatia kipato kizuri.
Picha na Martin Kabemba
 Watalii wakiogelea kwenye bahari ya Hindi ukanda wa Fumba ambao wageni wengi hufurahia sana kila wanapotembelea ukanda huo kisiwani Zanzibar.
Picha na Martin Kabemba
Watoto wa Mwanyanya Zanzibar bila kuogopa athari inayoweza kuwapata ya maradhi, wakiogelea kwenye madimbwi ya maji yanayotokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kisiwani zanzibar hivi sasa.
Picha na Martin Kabemba

2 comments:

  1. Miaka 73 bado ana biceps za nguvu - kazi za suluba hizo. Mlioko Ughaibuni tayari mmeshapelekwa nursing homes, Mzee Omar ndio kwanza anapeta

    ReplyDelete
  2. I love the stress free smile of wakulima wa mwani

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.