Habari za Punde

Matukio ya Harakati katika Kisiwa cha Zenji...

Mdau wangu kama bado hujapata kutembelea mitaa ya Mji Mkongwe ukaona harakati zake wakati wa asubuhi mpaka mchana utafikiri watu hawa watakuwa katika eneo hilo mpka usiku lakini hivyo sivyo mdau wangu,
 
Sehemu hii huwa na harakati za hapa na pale kwa Wafanyabiashara mbalimbali hufika katika eneo hili kwa ajili ya Biashara zao na ikifika wakati wa jioni kila mmoja hurudi sehemu yake ya makaazi , Eneo hilo huwa na mvuto kwa watu wanaotembelea katika Visiwa vya Zanzibar na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika mji huu.
 
Kwa Biashara za kila aina ulipita huku utaona biashara ya dagaa wakavu , wauza tende, wauza kofia za kiua sehemu hii ni maarufu kwa biashara ya Kofia za Kiua katika jumba la historia maarufu huitwa jumba la Treni Darajani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.