Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.{Picha na Ali Meja]
Na Lulu
Mussa
Akifungua kikao kazi, Eng. Mwihava
amesema, Tanzania iliridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanuai mwezi
machi , 1996 na kufuatiwa na Mkutano wa
wanachama ulioazimia kuandaa itifaki kuhusu
usalama wa Mazingira dhidi ya Athari za Bioteknolojia ya Kisasa.
Itifaki hiyo pamoja na mambo mengine inasisitiza
nchi wanachama kuandaa Sheria na kuweka mfumo na mwongozo wa Usimamizi salama
wa Mazingira na kulinda afya ya binadamu, bioanuai na wanyama.
Aidha, lengo la teknolojia ya Kisasa
ni kukidhi haja ya kuimarisha ubora, kudhibiti magonjwa, kuhimili ukame na
kukuza uzalishaji. Hata hivyo imebainika kuwa bado kuna wasiwasi wa athari
zinazoweza kupatikana kutokana na teknolojia hiyo endapo itatumiwa bila kufuata
utaratibu. “kwa hiyo tumewaita ili kujadili na kutoa maoni kuhusu utekelezaji
wa Kanuni hizi ili tupate mwelekeo wa suala hili na kuishauri Serikali’. Alisisitiza
Eng. Mwihava.
Akitoa maezo ya awali, Mkurugenzi wa
Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu amesema kuwa
lengo la kanuni hizo si kuzuia au kukwamisha matumizi ya Bioteknojia hapa
nchini bali ni kuhakikisha nchi inanufaika na matumizi hayo kwa kuzingatia
usalama wa afya ya binadamu na Mazingira.
Aidha baadhi ya wadau katika kikao
hicho walikuwa na maoni tofauti na kuitaka Serikali kupitia upya kanuni na kufanya
tathmini ya kuondoa ama kuacha kuondoa kipengele cha Strict liability.
Mkutano huo umehusisha wanasheria,
wanasayansi, Mtandao wa wawakilishi wa wakulima na Taasisi za Utafiti za Mbegu,
hususan Pamba na Mahindi.
No comments:
Post a Comment