Habari za Punde

Jaji Bomani ashauri ipigwe kura ya maoni ili kubaini mfumo wa muungano

NA BELINDA KWEKA – MAELEZO,DSJ
MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali  mstaafu, Jaji Mack Bomani ametoa wito wa kupigwa kwa kura ya maoni kwa wakazi wa Tanzania Visiwani ili kuona kama wanahitaji mfumo gani wa Muungano kabla ya kuendelea na mchakato wa sasa wa rasimu ya Katiba  mpya .
 
Akizungumza na  waandishi wa  habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO , Jaji Mack   Bomani  alisema  anaipongeza tume ya Jaji  Joseph   Warioba kwa kazi nzuri na pia kwa mapendekezo yake juu ya  Muungano  wa Tanzania.
Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo  Jaji  Bomani  alitoa historia fupi juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo ameeleza kuwa muungano huo ulipendekezwa na hayati Sheikh Abeid  Amani  Karume na hayati Mwalimu  Julius  Nyerere, ambao walikutana mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari, mwaka 1964.
 
Jaji Bomani   aliongeza  hayati  Karume  alipendelea nchi mbili kuungana  na kuwa  nchi moja , lakini hayati  Nyerere  alisita  kidogo  kwa kuogopa kwamba ingeonekana Zanzibar imemezwa na Tanganyika na pengine kuleta maasi Zanzibar hivyo kupendekeza kuundwa mfumo wa muda mfupi wakati mfumo wa kudumu ukifanyiwa kazi.

“Suala la Muungano  ndilo  suala kubwa kuliko yote katika  mchakato  wa Katiba mpya.  Niliwahi kuto ushauri nao ni kwamba ifanyike kura ya maoni ya wananchi hasa Zanzibar  kama wanautaka muungano au la na kama wanautaka uwe muungano  wa mfumo gani ? Mpaka sasa maoni ambayo yanasikika ni maoni ya viongozi mara Zanzibar ijitoe kwenye muungano mara tuwe na muungano wa mkataba,” alisema  Jaji Bomani.
 
Akijibu maswali aliyoulizwa  na waandishi wa habari ,Jaji Mack Bomani amesema katika uundwaji wa Serikali tatu anaamini utaweza kumaliza migogoro inayojitokeza mara kwa mara hasa upande wa Zanzibar kuogopa kumezwa. “Woga  wa gharama za mfumo wa Serikali tatu hauna msingi.Inategemea Serikali hizo unazifanya vipi.ipo mifano mingi mno duniani ya miungano ya mfumo mbalimbali,” alisisitiza.
 
Pia ameongezea kuwa kama kutaundwa Serikali tatu basi iwe Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano.
 
Akiongezea kuhusu katiba mpya amesema “kwa maoni yangu si lazima kazi hii ya katiba iishe kabla ya 2015, tupate muda wa kutosha ili tuweze kupata katiba ya kueleweka na kukubalika na kila mtu”.

8 comments:

  1. habari nyengine ni chumvi tu, si kweli kuwa karume alitaka kuunganisha nchi ziwe moja, na hata kama alitaka yeye hawezi kuwakilisha matakwa ya maelfu ya wananchi wa zanzibar, serikali tatu hatuzitaki kaa nazo mwenyewe , tunataka zanzibar huru , na kuwe na maeneo ya ushirikiano tu baina yetu na watanganyika , kila mmoja aangalie nchi yake, vile vile tunataka mturudishie mwambao wote wa pwani amabo ulikuwa katika himaya za zanzibar ,

    ReplyDelete
  2. ukweli ni kwamba mapinduzi yalifanywa na nyerere ili aweze kuitawala zanzibar na kuua uislamu ktk visiwa hivi ambavyo vilionekana ni tishio kwa watu wa mataifa ya magharibi ( sielewi kwa nini hawa watu hawajiamini na imani zao ) ambao walimshawishi nyerere kupanga njama za mapinduzi ili baadae afanye huo muungano ili aweze kuwadhibiti waisilamu. Huu muungano kwa ukweli unalazimishwa na watu wa mataifa ya nje , lakini tukumbuke tukianza kuuwana hapa wao watakuwa hawapo. Nakubaliana na kura ya maoni tuone wanafiki wangapi wantaka huu muungano, na waadilifu wangapi hawataki.

    ReplyDelete
  3. Mapinduzi na muungano ni matokeo ya 'ukhanithi' waliokua wakiufanya Waarabu dhidi ya W'bari wenzao wasio na asili za kiarabu.

    Na hata leo hii, hofu kubwa tuliyonanyo juu ya kuvunjika muungano ni kujirudia kwa tabia za kipumbavu tulizoziondoa 1964.

    Hivi inakuwaje UWAMSHO kumuona kila M'bari asiye na asili ya kiarabu kua ni mgeni Z'bar, wakati wale wenye asili hizo wakionekana kua ndio wenyeji?

    Wazee wetu waliwapokea wamanga kutoka kwao enzi hizo 'tongo' tupu na majambia wanatafuta kazi za ulinzi kwenye mabanda ya karafuu..leo hii kibao kimegeuka..eti sisi ndio wageni!

    Tunasema kinywa 'kipana' kupata Z'bar huru ni kitu kimoja na kuweza kuitawala kama mnavyotaka nyinyi ni kitu kingine!

    ReplyDelete
  4. @Anonymous wa kwanza.

    Naunga mkono madai ya maili zetu 10, ndani ya mwambao kama zilivyo ainisha kwenye Berlin conference of 1884-85!

    Hata hivyo, changamoto inabaki kwa mfano tukipewa tutaishije na WAZARAMO, WANDENGEREKO, WAMATUMBI, WACHOLE, WAMAKONDE N.K.?

    Ambao, pamoja na kuchangia historia inayofanana kama vile USHIRAZI, UISLAMU NA USWAHILI, kikundi cha UWAMSHO wanawaona WABARA, WAGENI na MAKAFIRI?

    ReplyDelete
  5. naona hap wachangiaji wengine kama wanachanganya habari , kwani nani kasema ukivunjika muungano, uamsho ndio watakuwa serikali? kwani kina Dr Sheni na sefu ni uamsho? naomba nielimishwe. kasumba za ubguzi wa rangi naona zimepamba moto katika karne hii ya 21 bado tu? kwani Dr Sheni ni muarabu? naovoelewa mimi kuwa tukipata uhuru serikali iliyopo itaendelea kutawala kama kawaida mpaka uchaguzi mwengine utapofika. tafadhalini msiwapeleke mchomo wananchi kwa kuwapumbaza. Uhuru wa zanzibar umefika sasa , tusirudi nyuma kwa kubaguana , hizi mbegu mbovu za ubaguzi zimepandikizwa na watanganyika kwa faida yao, zanzibar ni nchi ya watu rangi zote, angalia marekani nani anatawala sasa? mzungu? jee mtasema nini ? muhimu yoyote anayetawala awe na uchungu na nchi na kuiletea maendeleo bila kujali rangi yake ili mradi awe mzanzibari.

    ReplyDelete
  6. Anonymous wa 2,34..Nyinyi hamujenda chool nini.. Munachukia Waarabu na Hao Ma-babazenu akinaSeifu Ali Iddi ndio taa zao (usiku) wakati umeme ukiwa ni wa Mgao.?
    Hivyo Muamsho ni waarabu gani wale? Kwakua mumemuona Shekh Farid na Shekh Azan ambao wazee wao ni Waswahili waliochanganya damu na warabu? Mbona Bukoba na Mwanza muko na watu wenye Rangi kama Shekh Faridi.. ? Au Ndio munawauwa kwakufanya Dawa za Uchawi? ...Kwasababu munaon watakuja kuitawala Tanganyika?...

    Wacheni Ujinga huo ati wanaleta Waarabu ..waarabu mbona munakwenda kuposa hao hao waarabu na hamwendi kuo Wamasai Wenzenu Washenzi nyinyi.

    Zanzibar kuwa Huru sio Suala la Waarabu bali ni Suala la Wazanzibari wenyewe. Hata kama watatawaliwa na huyo Murabu munayemuona nyinyi (Ukiona Chongo ) wameshaweza kupambanu baina yakutawaliwa na TWANA lisilo na Mila dini Imani wal Utamaduni.. kulikokutawaliwa na Waarabu.

    Kama Sio wao Waarabu wa Omani tungekua tunauwana kwa mapanga kama Tanganyika.. Lakini Namshukuru Allah wametuletea Dinio ya Kiislamu ambayo inatufundisha jinsi yakua na Imani, utamaduni na Ustarabu...I feel proud to be a muslim & Zanzibari.

    ReplyDelete
  7. @ Anonymous wa sita.
    Kwa taarifa yako Uislamu na ustaarabu Z'bar haukuletwa na Waomani, bali washirazi kutoka kusini ya Iran.

    Fuatilia vizuri historia ya akina MWINYI MKUU(DUNGA), MKAMANDUME(PUJINI PEMBA)na MWANA WA MWANA (TUMBATU).

    Sayyid SAID na alikuja hapa kwa utawala tu, na histori yake ya utawala hata huko OMAN ilitokana na kuuwa.

    Kumbe wageni wa Z'bar hawatoki Tanganyika peke yake na Uarabu wanatoka ndio maana hata historia ya hapa huijui.

    Fuatilia vizuri tafsiri ya maneno MTWANA na MSHENZI isije ikawa na familia yako imo!

    ReplyDelete
  8. hAWA WANA ONAONESHA USTARAU WAO MDOGO WAKIPATA HAO UAMSHO INA ONESHA HAPATOKALIKA, HAPA, ZBAR, KAMA HAMTAKI MADARAKA NA RAIS SHEN, HAJAKUTUMENI, MUUVUNJE, MUUNGANO WETU, NA NDUGU ZETU, KAMA KUPUMUA NIKULE, KUCHOMA BARABARA, NA KUTUPIGISHA VIGONGONA MABOM YAMACHOZI,,HATUTIKI,TUNA ULIZAKWANINI, PEMBE HAKUNA UAMSHO, NIFITINA ZENU KWA KUWA MNALETEWA PESA NA MABWANA ZENU, WAKIMANGA, MNATAKA KUITIA ZIKI UNGUJA, WAZEE WENU WAKO KWENU HAPA MNALETA FUJO BURE

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.