Habari za Punde

Mnada wa Samaki Marikiti Darajani.


 Dalali wa mnada wa samaki akinadi samaki aina ya Taa katika marikiti ya Darajani kipande kimoja cha Taa kiliuzwa kwa shilingi 70,000/= katika mnada huo.
Watowa huduma ya upasuaji wa samaki wakubwa katika soko la marikiti wakipasua samaki aina ya Taa kwa ajili ya kuuzwa kwa Wachuuzi katikamarikiti hiyo.

2 comments:

  1. Asante kwa mara nyingine kutonesha jinsi Nyumbani hali halisi ivyobakia kama ilivyokuwa miaka ya 80 mwishoni mwa miaka ya 70 hadi kufikia mwazoni mwa miaka ya 80 nikiwa kijana niliyekuwa nasoma skuli ya Vikokotoni, hali ya marikiti ya samaki ipo hivyo na hadi leo ipo vile vile,hii tunaingia na viatu kama tujuwavyo kiatu kinachukuwa kila kitu njiani Mmungu mrahamu mwalimu wangu Mkuu mali Khalfan

    ReplyDelete
  2. Baada ya miaka 50 ya uhuru Z'bar bado haina ustaarabu ktk suala la masoko

    Samaki wanatayarishwa na kuuzwa popote bila kujali afya za watumiaji.

    Baya zaidi ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba soko au muuzaji wa samaki lazma anuke vumba!

    Aibu nyengine ya mwaka ni kwamba Z'bar imebaki sehemu pekee A'mashariki ambapo samaki hawapimwi kwa kilo bali kwa macho!

    Ndio maana mimi husema, kwetu sisi kusoma ni kuharibu pesa tu kwa vile jamii yetu haibadiliki

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.