Na Mwantanga Ame
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Zanzibar Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu, amevitaka vyombo vya dola kuwadhibiti viongozi dini wanaotumia misikiti kutoa ushawishi kwa vijana kufanya vurugu.
Katibu huyo, aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jana katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja
Alisema Katibu huyo, Zanzibar hivi sasa, imo katika utekelezaji wa serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo haitakiwi kwa viongozi hao kuanza kutumiwa majukwaa ya dini kuhamasisha vijana kufanya vurugu jambo ambalo linaweza likasababisha kutokea kwa migongano na kuharibu amani ya nchi.
Alisema inasikitisha kuona hivi karibuni kuwapo kwa Sheikh Ponda Issa Ponda alipita na kutoa mihadhara ya kuhamasiasha chuki za kidini na utengano kwa kuwashawishi wananchi waingie barabarani ili kufanya kufanya fujo na ghasia.
Waride alisema hotuba za Sheikh Ponda alizozitoa kwa nyakati tofauti kwenye misikiti ya Mbuyuni,Kwarara na Nungwi kisiwani Unguja kimsingi zinapanda mbegu za chuki, kuondosha upendo pia kuhatarisha amani na kuchochea umwagaji wa damu.
Alisema matamshi yake ni hatarishi kwa amani na utulivu uliopo kwani alidai anawataka waumini wa kupigania jihadi na kushiriki harakati za kuikomboa Zanzibar akidai serikali iliyopo madarakani inawakandamiza na kuwanyanyasa wananchi.
“Sheikh Ponda ni hatari, anapita akipanda shari, hasama na chuki miongoni mwa wananchi, anahamasisha wananchi wafanye uasi, kulipiza visiasi na kutaka waingie barabarani kwa maanadano ya kutetea haki kama ilivyo Misri ”Alisema Waride.
Aidha alisema CCM kwa upande wake imeshangazwa na ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama wa raia kumtazama macho shehe huyo bila ya kumchukulia hatua za kishria huku akiwatukana matusi ya ngu0ni viongozi wa kiserikali waliochaguliwa kwa mujibu wa katiba na sheria.
Katibu huyo wa Idara ya Itikadi na Uenezi alimtaja Sheikh Ponda kuwa bila shaka anatumiwa na mtandao wa wa vurugu ili kuharibu na kuvuruga amani na hamu yake ni kuona damu ya wananchi ikimwagika na nchi ikiingia kwenye machafuko.
“Panapofuka moshi chini kuna moto, mambo yote hatari huanza kidogokidogo na kukomaa, anayoyafanya Ponda yakipevuka yataleta maafa, majanga na kutoweka kwa amani nchini , kinga ni bora kuliko tiba ”Alisema Waride.
Alisema kitendo chake cha kulitumia jukwaa la dini na kufanya siasa misikitini hakikubaliki na kwamba kikiachiwa kiendelee kinaweza kuleta maadhara na mgawanyiko wa kijamii hatimae kuiingiza nchi katika mapigano.
Waride akitolea mfano wa ghasia na vurugu zilizofanywana na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho mwezi Mei na Oktoba mwaka jana ziliweza kuiletea hasara Serikali na kuipotezea kiasi cha shilingi biliono moja kutokana na mapato ya uatlii.
“Ghasia za uamsho ziliipotezea Serikali ya Zanzibar fedha nyingi, sekta ya utalii huchangia kwa asilimia 83 na pato la Taifa kwa asilimia 25, watalii walikataa kuja Zanzibar kutoakan na ghasia zilizokuwepo, Ponda amekusudia shari na hapaswi kutazamwa macho”Aliongeza kusema Waride.
Alisema uamuzi wa Sheikh Ponda kuweka dago Zanzibar unaweza kuhatarisha maelewano yaliopo na kuivuruga Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo imekuwa ikifanya kazi pamoja chini ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein tokea ilipoundwa mwaka 2010.
Nadhani Mh. Waride hajui alisemalo, suala la kutenganisha dini na siasa tayari limeshashindikana!
ReplyDeleteWakati wenzetu wanatumia makanisa kuifitinisha CCM dhidi ya CHADEMA Mh. yeye sijui anataka viongozi wetu wafanyeje?
CHADEMA, wamesimamisha Padri Dr.Slaa kuwa mgombea urais, mch. Isreal natse(mbunge) Mch. Peter msigwa(mbunge) na madiwani wa kumwaga wachungaji na wote wanahubiri makanisani Bi waride yeye anataka waislamu wazidi kulala.
Suala la Ponda lisifananishwe na UWAMSHO. uwamsho ni WAHUNI wanaotaka kugawa nchi wakati PONDA ni kiongozi wa dini anaetetea maslahi ya waislamu.
Juhudi za ponda tayari zimeanza kuzaa matunda ktk maeneombali mbali ya ajira hasa Tza Bara.
na wewe umeingia katika genge la waride moja kwa moja,watetezi wa zanzibar sio wahuni bali nyie ndio wahuni
ReplyDelete