Habari za Punde

PBZ Yashinda katika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha, Uwekezaji na Uwezeshaji kwa Wote Tanzania.

Msaidizi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ame Haji Makame akiinua Kombe la Ushindi Juu kuwaonesha Wafanyakazi wa PBZ kabla ya kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour wakati wa sherehe za kusherehekea ushindi huo uliofanyika katika Makao Makuu ya PBZ Islamic Bank Mpirani jengo la Bima.
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Amour, akikabidhiwa Kombe la Ushindi la Wiki ya Huduma za Kifedha, Uwekezaji na Uwezeshaji kwa Wote , kutoka kwa Msaidizi Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ame Haji Makame, PBZ imeshika nafasi ya kwanza katika maonesho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja na kushirikisha Taasisi zinazoshughulika na Fedha Tanzania. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Benki ya PBZ Islamic Mpirani

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya PBZ hadi kushinda maonesho ya Taasisi za Fedha Tanzania katika maonesho yaliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar-es- Salaam na PBZ kuibuka mshindi wa kwanza katika maonesho hayo
Mwakurugenzi wa Idara mbalimbali za PBZ wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Makao Makuu ya PBZ Islamic katika Jengo la Bima Mpirani Zanzibar.
Wakurugenzi wa Idara za PBZ wakifuatilia mazungumzo na Waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano katika jengo la Makao Makuu ya PBZ Islamic mpirani.
Wakurugenzi wakifuatilia maswali ya waandishi wa habari wakati wa kutambulishi ushindi wao.
Mwandishi wa habari akiuliza swali kuhusiana na maendeleo ya kuboresha huduma za PBZ kwa wateja wake na mafanikio ya zoezi lake la kutowa mikopo kwa Wananchi.

                        Wakurugenzi wa PBZ wakifuatilia maswali ya waandishi na kuweka kumbukumbu yao


Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akijibu maswali ya waandishi wa habari katika sherehe za kutambulisha ushindi wao walioupata katika maonesho ya Taasisi zinazojishughulisha na huduma za Fedha Tanzania, yaliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar-es-Salaam.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.