Habari za Punde

Jamii Yatakiwa Kutowatelekeza Wazee.

Na Mwanajuma Mmanga
JAMII imeshauriwa kutowatelekeza wazee badala yake wathamini michango yao kwa ujenzi wa familia bora na taifa.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Mahmoud Muhammed Mussa kwa niaba ya Spika, alipokuwa kizungumza na wazee katika kilele cha siku ya wazee duniani zilizofanyika Sebleni.

Alisema ni vyema jamii ikawatunza na kuwalea wazee wao kwani kazi ya kulea sio kazi ya serikali.

Aidha alisema majirani nao wana nafasi kubwa ya matunzo kwa wazee wanaoishi kwenye mitaa yao pale wanapoona wanayumba kimaisha.

Alisema serikali itaanzisha mfuko maalum wa wazee ili kuwaendeleza na kuachana na omba omba.

Katibu Mkuu wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Maendeleo Wanawake na Watoto, Msham Abdalla Khamis kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Zainab Omar Mohammed, alisema serikali imeaandaa sera ya hifadhi ya jamii inayolenga kusaidia wazee na makundi mengine katika jamii.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wastaafu na wazee Zanzibar, Nd. Masruru Said Ferouz akisoma risala kwa niaba ya wazee, alisema serikali itoe nafasi kwa wazee katika vyombo vya maamuzi.

1 comment:

  1. Tusome hii ili tuwashughulikie wazee wetu na sio kuwa maneno matupu tu!

    http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2013/10/jamani-lets-copy-this.html

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.