Watanzania waishio Johannesburg wanawatafuta ndugu, rafiki au jamaa wa Shiraz Abeid Juma (pichani), ambaye sasa ni marehemu. Shiraz alifariki wiki hii na kuzikwa siku ya Jumanne huko Johannesburg, Afrika Kusini.
Marehemu alifika Afrika Kusini akitokea eneo la Mpendae kule Zanzibar kama nyaraka alizoacha zinavyoonyesha. Namba za simu zilizokuwa kwenye vitabu vya marehemu hazipatikani. Kwa yoyote mwenye kumfahamu marehemu, tafadhali wasiliana na Abdallah Hussein +27 71 216 8505.
No comments:
Post a Comment