Habari za Punde

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu CUF Azungumza na Waandishi.

Na Ramadhani Ali  Maelezo Zanzibar                              
Chama cha Wananchi (CUF) kimeilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutokana na jinsi ilivyosimamia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika tarehe 2 mwezi huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya CUF, Vuga Mjini Zanzibar leo, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa Chama hicho Salim Bimani amesema Uchaguzi huo haukuwa huru na haukuwa wa haki.

Amesema vitendo vya  kuvurugwa uchaguzi huo vilianza kujitokeza kuanzia  wakati wa  kampeni na siku ya uchaguzi lakini pamoja na kutoa taarifa kwa Tume ya Uchaguzi hakuna hatua yoyote iliyochukua.

‘’Chama cha CUF kilibaini tokea mapema maandalizi ya fujo na matumizi mabaya ya nguvu za dola pamoja na Vikosi vya Serikali, ambavyo viliandaliwa kwa dhamira ya makusudi ya kuwapa haki wasiostahiki na pia kuwanyima watu wengi haki yao ya kufanya maamuzi ya kidemokrasi’’, alisema Salim  Bimani.

Aliongeza kuwa upo ushahidi kwamba Vikosi vilitumika kuwalinda na kuwasafirisha wapigakura mamluki kutoka sehemu  nyengine kuja kupiga kura  bila ya hatua yopyote ya kisheria kuchukuliwa.

Bimani alidai kuwa vikosi hivyo vilithubutu kuwatisha  baadhi ya wananchi waliopaza sauti kupinga mwenendo huo haramu wa uchaguzi.

“ Wananchi na Chama cha Wananchi, CUF , walijenga matumaini makubwa ya kuona Uchaguzi huru na wa haki ukifanyika katika zama hizi ambazo Zanzibar inaongozwa na Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chini ya misingi ya maradhiano ya kisiasa, inayozingatia amani, utulivu, demokrasi na mshikamano kupitia siasa za kistaarabu’’, aliongeza Mkurugenzi  Bimani .


Alisema kutokana na kasoro nyingi katika uchaguzi huo mdogo, CUF imekosa imani na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Daftari la Kudumu la wapigakura kutokana na kuchezewa na halipo kwa misingi ya kutekeleza demokrasia, Haki na Uadilifu.

Bimani alirejea kauli ya Chama hicho kutaka Tume ya Uchaguzi (ZEC) ivunjwe ili kutoa fursa ya kupatikana Mamlaka nyengine huru itakayoweza kusimamia Uchaguzi wa Haki na wa Kidemokrasia.

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki ulifanyika kufuati  kujiuzulu aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid mwishoni mwa mwaka jana.

8 comments:

  1. CCM washakujuweni udhaifu wenu upo wapo. Mumeshindwa kujifunza ya Bububu. Sasa imebaki blah blah blah. Mulitegemea Mapuri afanye nini. Wajumbe wenu kwenye tume ya uchaguzi ni feki. Sheria na uundwaji wa tume hii ni kwa maslahi ya chama tawala. Mambo yenu ni kusubiri ushahidi kamili Tu. Wakeup!!!!

    ReplyDelete
  2. ndugu CUF hakuna kitu kwa kura hapa znz , demokrasia ipo kwenye vitabu na mdomoni sio kivitendo , kama hamkushika mtutu sahauni kupata chochote ,

    ReplyDelete
  3. viongozi wote wa juu cuf sio wabunifu wa kupanga mipango endelevu ,kujifunza mambo mbali mbali kuhusu chaguzi zanzibar,wanalojua wao ni kupiga makelele tu,tulianza uchaguzi wa vyama 1995,2000,2005,2100 mpaka leo hawajajua dawa za chaguzi zilizopita,ccm sio watu wa kuwachekea,wako kama wanga mchana binadamu usiku wachawi na majini wala watu,naamini kama viongozi wa cuf wangekuwa kama wa chadema hakika zanzibar ingekwisha komboka kutoka kwa mkoloni mweusi

    ReplyDelete
  4. SALIM BIMAN NI MMJOA WA VIONGIZI KELELE MAJIGAMBO BILA VITENDO, KILA SIKU HAMNA IMANI NA TUME,KWANI KUSUSIA UCHAGUZI KUTAKUWA NA HASARA GANI,CUF NI CHAMA CHA MAYAHE,HEWALA BWANA,TUNATAKA HILE CUF NGANGARI YA 1995 ...HALAFU USIKIE HAO MACCM KAMA HATATAFUTA NCHI YAO

    ReplyDelete
  5. CUF ni chama cha longolongo! Hakina moja wala mbili. Kazi yao ni kuusaliti umma wa Zanzibar kwa kuwambia uongo usikokwisha. Mjinga hajifunzi kutokana na makosa yake. Msininukuu

    ReplyDelete
  6. KUNA MZEE MMOJA ZAMANI ALINIAMBIA MANENO NA AMESHATANGULIA KWENYE HAKI KUWA ZANZIBAR TATIZO KUBWA NI WAZANZIBARI HAWAPENDANI WALA HAWAONEANI HURUMA,PIA HUSALI SALA TANO LAKINI MMOJA AKIPATA NAFASI HUMUUZA MWEZIWE KWA BEI POA.
    SITOMSAHAU MZEE HUYU KWANI HIVI SASA NAONA VIONGOZI WA ZANZIBAR WA JUU WANAVYOIUZA ZANZIBAR KWA BEI POA HUKO TANGANYIKA HAWAONI HAYA WALA VIBAYA SASA KISHINDO KINAKUJA WATANGANYIKA HAWATAKI WANATAKA TANGANYIKA YAO IFUFUKE,NA WAZANZIBARI HAWATAKI WANATAKA TANGANYIKA IENDELEE KUFA NA KERO ZA MUUNGANO ZIDUMU.
    SASA KAMA HUU SI UNAFIKI NINI?
    KAMA HIZI SI NJAA NINI?
    KAMA KWA LUGHA TULIYOIZOEA HAPA KWETU AMBAYO SI MATUSI HUU SI UHANISI NINI?
    HAWA NDIO WAZANZIBARI NINAOWAJUA MIMI NILIOMBIWA NA MZEE WANGU AMBAE NI MARHUM SASA.
    ASANTE.

    ReplyDelete
  7. Mapuri weeeeeeeeeeeeeee!!!!!

    ReplyDelete
  8. KUNA MZEE MMOJA ZAMANI ALINIAMBIA MANENO NA AMESHATANGULIA KWENYE HAKI KUWA ZANZIBAR TATIZO KUBWA NI WAZANZIBARI HAWAPENDANI WALA HAWAONEANI HURUMA,PIA HUSALI SALA TANO LAKINI MMOJA AKIPATA NAFASI HUMUUZA MWEZIWE KWA BEI POA.
    SITOMSAHAU MZEE HUYU KWANI HIVI SASA NAONA VIONGOZI WA ZANZIBAR WA JUU WANAVYOIUZA ZANZIBAR KWA BEI POA HUKO TANGANYIKA HAWAONI HAYA WALA VIBAYA SASA KISHINDO KINAKUJA WATANGANYIKA HAWATAKI WANATAKA TANGANYIKA YAO IFUFUKE,NA WAZANZIBARI HAWATAKI WANATAKA TANGANYIKA IENDELEE KUFA NA KERO ZA MUUNGANO ZIDUMU.
    SASA KAMA HUU SI UNAFIKI NINI?
    KAMA HIZI SI NJAA NINI?

    HAWA NDIO WAZANZIBARI NINAOWAJUA MIMI NILIOMBIWA NA MZEE WANGU AMBAE NI MARHUM SASA.
    ASANTE.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.