THE UNITED REPUBLIC
OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI
WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
UTANGULIZI
1.
Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa
na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka
ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa
kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu
cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na
mahali anapotoka mjumbe husika.
2.
Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa
Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i)
Wabunge
wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)
Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)
Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3.
Makundi
hayo ni kama ifuatavyo:-
(i)
Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii)
Taasisi za Kidini (20)
(iii)
Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
(42);
(iv)
Taasisi za Elimu (20);
(v)
Watu wenye Ulemavu (20);
(vi)
Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii)
Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)
Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix)
Vyama vya Wakulima (20); na
(x)
Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana
(20).
4.
Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo
la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo
la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza
ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina
kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko
lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na
mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5.
Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande
wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa
kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
6.
Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka
Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao . Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na
kwa upande wa Zanzibar
mapendekezo hayo yalihusisha watu 874.
Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria,
watu 118 walijipendekeza wenyewe na
kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7.
Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa
katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
Na.
|
Kundi/Taasisi
|
Taasisi zilizoleta mapendekezo
|
Idadi
ya Watu Waliopendekezwa
|
Idadi
ya Wajumbe Wanaotakiwa
|
Idadi
ya Walioteuliwa
|
|||
1.
|
Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
|
246
|
98
|
1,203
|
444
|
20
|
13
|
7
|
2.
|
Taasisi za Kidini
|
55
|
17
|
344
|
85
|
20
|
13
|
7
|
3.
|
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
|
21
|
14
|
129
|
69
|
42
|
28
|
14
|
4.
|
Taasisi za Elimu
|
9
|
9
|
84
|
46
|
20
|
13
|
7
|
5.
|
Makundi ya Walemavu
|
24
|
6
|
97
|
43
|
20
|
13
|
7
|
6.
|
Vyama vya Wafanyakazi
|
20
|
1
|
89
|
13
|
19
|
13
|
6
|
7.
|
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
|
8
|
1
|
43
|
4
|
10
|
7
|
3
|
8.
|
Vyama vinavyowakilisha Wavuvi
|
7
|
3
|
45
|
12
|
10
|
7
|
3
|
9.
|
Vyama vya Wakulima
|
22
|
8
|
115
|
44
|
20
|
13
|
7
|
10.
|
Makundi yenye Malengo Yanayofanana
|
142
|
21
|
613
|
114
|
20
|
14
|
6
|
Mapendekezo Binafsi
|
-
|
-
|
118
|
-
|
||||
Jumla
|
672
|
178
|
2,880
|
874
|
201
|
134
|
67
|
|
Jumla
Kuu
|
850
|
3,754
|
8.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka
masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe
wasiopungua theluthi moja wanatakiwa
kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania
Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201,
wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha,
mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya
wananchi wa Tanzania
kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika
mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe
201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na
nafasi zilizopo.
9.
Kama
nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar , majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza
ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za
kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar , taasisi zisizokuwa za kiserikali
zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
WAJUMBE
WA BUNGE LA KATIBA
10. Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
wakishirikiana na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe
walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a)
Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika
zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati
miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani
miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)
Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa
ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha
hii wajumbe wanawake ni 100 na
wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani
kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c)
Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji
kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa
kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42
wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila
chama.
Baada ya maelezo hayo
ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:
TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Magdalena
Rwebangira
|
2.
Kingunge
Ngombale Mwiru
|
3. Asha D. Mtwangi
|
4.
Maria Sarungi
Tsehai
|
5. Paul Kimiti
|
6.
Valerie N. Msoka
|
7. Fortunate Moses
Kabeja
|
8.
Sixtus Raphael Mapunda
|
9. Elizabeth Maro Minde
|
10. Happiness Samson
Sengi
|
11. Evod Herman Mmanda
|
12. Godfrey Simbeye
|
13. Mary Paul Daffa
|
|
1.
Idrissa Kitwana Mustafa
|
2.
Siti Abbas Ali
|
3.
Abdalla Abass Omar
|
4.
Salama Aboud Talib
|
5.
Juma Bakari Alawi
|
6.
Salma Hamoud Said
|
7.
Adila Hilali Vuai
|
|
TAASISI ZA
KIDINI- (WAJUMBE 20)
|
|
1.
Tamrina Manzi
|
2.
Olive Damian Luwena
|
3.
Shamim Khan
|
4.
Mchg. Ernest Kadiva
|
5.
Sheikh Hamid Masoud Jongo
|
6.
Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
|
7.
|
8.
Hamisi Ally Togwa
|
9.
Askofu Amos J. Muhagachi
|
10.
Easter Msambazi
|
11. Mussa Yusuf
Kundecha
|
12.
Respa Adam Miguma
|
13. Prof. Costa Ricky
Mahalu
|
|
1.
Sheikh Thabit Nouman Jongo
|
2.
Suzana Peter Kunambi
|
3.
Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
|
4.
Fatma Mohammed Hassan
|
5.
Louis Majaliwa
|
6.
Yasmin Yusufali E. H alloo
|
7.
Thuwein Issa Thuwein
|
|
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
|
|
1.
Hashim Rungwe Spunda
|
2.
Thomas Magnus Mgoli
|
3.
Rashid Hashim Mtuta
|
4.
Shamsa Mwangunga
|
5.
Yusuf S. Manyanga
|
6.
Christopher Mtikila
|
7.
Bertha Ng’angompata
|
8.
Suzan Marwa
|
9.
Dominick Abraham Lyamchai
|
10.
Mbwana Salum Kibanda
|
11.
Peter Kuga Mziray
|
12.
Isaac Manjoba Cheyo
|
13.
Dr. Emmanuel John Makaidi
|
14.
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
|
15.
Modesta Kizito Ponera
|
16.
Prof. Abdallah Safari
|
17.
Salumu Seleman Ally
|
18.
James Kabalo Mapalala
|
19.
Mary Oswald Mpangala
|
20.
Mwaka Lameck Mgimwa
|
21.
Nancy S. Mrikaria
|
22.
Nakazael Lukio Tenga
|
23.
Fahmi Nasoro Dovutwa
|
24.
Costantine
Benjamini Akitanda
|
25.
Mary Moses Daudi
|
26.
|
27.
John Dustan Lifa Chipaka
|
28.
Rashid Mohamed Ligania Rai
|
1.
Ally Omar Juma
|
2.
Vuai Ali Vuai
|
3.
Mwanaidi Othman Twahir
|
4.
Jamila Abeid Saleh
|
5.
Mwanamrisho Juma Ahmed
|
6.
Juma Hamis Faki
|
7.
Tatu Mabrouk Haji
|
8.
Fat –Hiya Zahran Salum
|
9.
Hussein Juma
|
10.
Zeudi Mvano Abdullahi
|
11.
Juma Ally Khatibu
|
12.
Haji Ambar Khamis
|
13.
Khadija Abdallah Ahmed
|
14.
Rashid Yussuf Mchenga
|
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
|
|
1.
Dr. Suzan Kolimba
|
2. Prof. Esther
Daniel Mwaikambo
|
3.
Dr. Natujwa
Mvungi
|
4. Prof. Romuald
Haule
|
5.
Dr. Domitila A.R. Bashemera
|
6. Dr. Jasmine
Bendantunguka Tiisekwa
|
7.
Prof. Bernadeta Kilian
|
8. Teddy Ladislaus
Patrick
|
9.
Dr. Francis Michael
|
10. Prof. Remmy J.
Assey
|
11.
Dr. Tulia Ackson
|
12.
Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
|
13.
Hamza Mustafa Njozi
|
|
1.
Makame Omar Makame
|
2.
Fatma Hamid Saleh
|
3.
Dr. Aley Soud Nassor
|
4.
Layla Ali Salum
|
5.
Dkt. Mwinyi Talib Haji
|
6.
Zeyana Mohamed Haji
|
7.
Ali Ahmed Uki
|
|
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
|
|
1.
Zuhura Musa Lusonge
|
2.
Frederick Msigala
|
3.
Amon Anastaz Mpanju
|
4.
Bure Zahran
|
5.
Edith Aron Dosha
|
6.
Vincent Venance Mzena
|
7.
Shida Salum Mohamed
|
8.
Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
|
9.
Elias Msiba Masamaki
|
10.
Faustina Jonathan Urassa
|
11.
Doroth Stephano Malelela
|
12.
John Josephat Ndumbaro
|
13.
Ernest Njama Kimaya
|
|
1.
Haidar Hashim Madeweyya
|
2.
Alli Omar Makame
|
3.
Adil Mohammed Ali
|
4.
Mwandawa Khamis Mohammed
|
5.
Salim Abdalla Salim
|
6.
Salma Haji Saadat
|
7.
Mwantatu Mbarak Khamis
|
|
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
|
|
1. Honorata Chitanda
|
2. Dr. Angelika
Semike
|
3. Ezekiah Tom
Oluoch
|
4. Adelgunda Michael
Mgaya
|
5. Dotto M. Biteko
|
6. Mary Gaspar
Makondo
|
7.
Halfani Shabani Muhogo
|
8.
Yusufu Omari Singo
|
9. Joyce Mwasha
|
10.
Amina Mweta
|
11.
Mbaraka Hussein Igangula
|
12.
Aina Shadrack Massawe
|
13.
Lucas Charles Malunde
|
|
1.
Khamis Mwinyi Mohamed
|
2.
Jina Hassan Silima
|
3.
Makame Launi Makame
|
4.
Asmahany Juma Ali
|
5.
Mwatoum Khamis Othman
|
6.
Rihi Haji Ali
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
|
|
1. William Tate
Olenasha
|
2. Makeresia Pawa
|
3. Mabagda Gesura
Mwataghu
|
4. Doreen Maro
|
5. Magret Nyaga
|
6. Hamis Mnondwa
|
7.
Ester Milimba Juma
|
|
1. Said Abdalla
Bakari
|
2. Mashavu Yahya
|
3. Zubeir Sufiani
Mkanga
|
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
|
|
1.
Hawa A. Mchafu
|
2.
Rebecca Masato
|
3.
Thomas Juma Minyaro
|
4.
Timtoza Bagambise
|
5.
Tedy Malulu
|
6.
Rebecca Bugingo
|
7. Omary S. Husseni
|
|
1.
Waziri Rajab
|
2.
Issa Ameir Suleiman
|
3.
Mohamed Abdallah Ahmed
|
VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
|
|
1. Agatha Harun Senyagwa
|
2. Veronica Sophu
|
3. Shaban Suleman
Muyombo
|
4. Catherine Gabriel
Sisuti
|
5.
Hamisi Hassani Dambaya
|
6.
Suzy Samson Laizer
|
7. Dr. Maselle
Zingura Maziku
|
8. Abdallah Mashausi
|
9. Hadijah Milawo
Kondo
|
10. Rehema Madusa
|
11.
Reuben R. Matango
|
12. Happy Suma
|
13.
Zainab Bakari Dihenga
|
|
1.
Saleh Moh’d Saleh
|
2.
Biubwa Yahya Othman
|
3. Khamis Mohammed
Salum
|
4. Khadija Nassor
Abdi
|
5. Fatma Haji Khamis
|
6. Asha Makungu
Othman
|
7.
Asya Filfil Thani
|
|
WATU
WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
|
|
1.
Dr. Christina Mnzava
|
2. Paulo Christian
Makonda
|
3.
Jesca Msambatavangu
|
4. Julius Mtatiro
|
5.
Katherin Saruni
|
6.
Abdallah Majura Bulembo
|
7.
Hemedi Abdallah Panzi
|
8. Dr. Zainab Amir
Gama
|
9.
Hassan Mohamed Wakasuvi
|
10.
Paulynus Raymond Mtendah
|
11.
Almasi Athuman Maige
|
12.
Pamela Simon Massay
|
13.
Kajubi Diocres Mukajangwa
|
14.
Kadari Singo
|
1.
Yussuf Omar Chunda
|
2.
Fatma Mussa Juma
|
3.
Prof. Abdul Sheriff
|
4.
Amina Abdulkadir Ali
|
5.
Shaka Hamdu Shaka
|
6.
Rehema Said Shamte
|
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
7
Februari, 2014
Haki haikutendeka. Hata Ofisi ya Rais wa Tanzania inashindwa kufanya haki? Raisi alipotoa mualiko wa makundi ya watu kuingia Bunge la katiba aliyataja makundi 10 na palitakiwa pajazwe chini ya makundi hayo. Matokeo eti kuna kundi la "mapendekezo binafsi" na wamekubalika wajumbe 118 kutoka Bara na visiwani hakuna maana yake hao wamepewa nafasi kuipendeleo na yasikitisha wote ni kutoka Bara. Mimi naona bora itangazwe wamepewa nafasi kiupendeleo au Rasi ajaze idadi hiyo hiyo kutoka visiwani.Kwanini ajaze nafasi ambayo hakuitangazaa?? Kwani kama ingelitangazwa nafasi hiyo jee wazanzibari wasingelijitokeza? "Hakiiiiii sawaaaa"!!!
ReplyDelete