Habari za Punde

Waziri Mbarouk ahimiza maendeleo chuo cha utalii

Na Ameir Khalid
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk, amelitaka baraza la chuo cha maendeleo ya hoteli na utalii ambalo limemaliza muda wake, kutoa michango na ushirikiano kwa baraza jipya ili kuendeleza mazuri yaliyofikiwa na chuo hicho.
Alisema baraza hilo lilifanya kazi nzuri kwa kushirikiana na uongozi wa chuo ambao umeleta ufanisi mkubwa.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuliaga baraza la chuo hicho, ilifanyika ukumbi wa chuo Maruhubi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho, Zulekha Kombo Khamis, alisema baraza hilo limefanikiwa kufanya mambo mbali mbali ya maendeleo ambayo chuo kinajivunia, ikiwa ni pomoja na kusaidia kupatikana jengo jipya la kisasa.
Pia alisema baraza hilo limeongoza katika mchakato wa kutaka kuunganishwa chuo hicho na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), hatua ambayo itaongeza heshima ya chuo.

Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa bazara lililomaliza muda wake, Khamis Mussa, ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kwa kuliunga mkono baraza lake katika kipindi chote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.