Na Hafsa Golo
Wachimba makaburi Mwanakwerekwe, wameiomba serikali na waumini wa dini
kulipatia hifadhi eneo hilo ili kudhibiti
vitendo vya kishirikina vinavyoendelea kufanya katika eneo hkithiri
katika eneo hilo.
Walisema hayo kwa nyakati
tofauti wakati wakizungumza na Zanzibar Leo.
Walisema njia muafaka ya
kuvidhibiti vitendo hivyo ni kumalizwa ujenzi wa uzio uliosita kwa muda mrefu
sasa.
Mchimba makaburi
aliejitambulisha kwa jina la Mohamed Nassour Juma (51) alisema, makaburi
yamekuwa yakifukuliwa na kuzikwa vitu mbali mbali vya kishirikina ikiwemo
vyungu,samaki waliofungwa kama sanda, mayai
na nazi.
Aidha alisema pamoja na
jitihada wanazochukua kuzuia vitendo hivyo, bado vimekuwa vikiendelea.
Alisema wakati wakichimba
makaburi wamekuwa wakikuta ndege ambao wamezikwa kama binaadamu.
Mchimbaji makaburi mwengine, Aboud
Jumbe Askar (29) alisema wamechoshwa na
vitendo vya kishirikiana vinavyofanywa hususan ndani ya makaburi.
Mkaazi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa
jina moja la Asha alikiri makaburi kutumiwa kwa imani za kishirikiana ambapo
mwanzo walikuwa na hofu lakini hofu hiyo sasa imeondoka.
Aliishauri viongozi wa siasa,wakiwemo
Wabunge na Wawakilishi kutafuta njia mbadala kuhakikisha uzio wa eneo hilo
unamalizika ili kupunguza vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment