Habari za Punde

Hospitali Mpya Binafsi ya Mwekezaji Mzalendo Mzanzibar kuzinduliwa Kesho.

Muonekano wa Jengo jipya la Hospitali lililojengwa na Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar inatarajiwa kufunguliwa kesho katika maeneo ya jirani na Wizara ya Afya Mnazi mmoja, jirani na Chuo cha Mwalim Bee majestiki Zenj.  

6 comments:

  1. kwa jengo linaonekana zuri sijui huduma tena?, mutafute madaktari bingwa sio muweke hao madaktari wa m/mmoja hawajui chochote kazi dharau tu, mukiweka ma DK wa maana basi tutakuja tu maana tushachoka kwanda bara kwanza unaumwa pili usafiri inakuwa balaa juu ya balaa

    ReplyDelete
  2. Kweli jengo kwa nje liko smart kabisa. Tunataka madaktari bingwa jamani tutakwenda kwa gharama yoyote kwani huko India tunakwenda. Kama alivyosema mdau hapo juu sio Wa M/mmoja Hawa nao pia ni mabingwa lakini bora waachwe Kule mnazi mmoja vyenginevyo kutakuwa hakuna tofauti. Ukienda hospitali nyingi za private madoctor ni hao hao wanaofanya mnazi mmoja sio tatizo sana kwani wanatafuta Riziki zao lakini kwa kwelu ufanusi khasa Wa utendaji ni mdogo pengine kwa sababu ya overload ya kazi. Naomba wahusika kwa hospital hoi tubadilike. Naitakia kila la kheri hospitali hii mpya ambayo inatupa matumaini mapya ya kupata huduma bora za Afya.

    ReplyDelete
  3. Haya ndio tunayoyataka khasa. Tunaiomba Serikali yetu tukufu ishajihishe zaidi hao wawekezaji kwenye sekta kama hii sio kwenye Utalii tu.

    ReplyDelete
  4. Kinachohitajika z'bar, sio uwekezaji tu bali pia uhuru wa kuwekeza. Nakumbuka mwekezaji wa hospitli ya Al -Rahma alikua na malengo makubwa lkn. alihofia sana ya kisiasa iliyokuwepo!

    Nakumbuka wakati fulani 'walipigwa mkwala' sana wakati walipowapokea majeruhi wa risasi wa chama cha upinzani. SASA

    Ktk hali kama hiyo, huwezi 'kurisk' uwekezaji mkubwa ktk afya hapa. bora hivo-hivo wagonjwa waelekee Bara au India mpaka pale tutakapopata akili nzuri!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.