Nimemjua Mzee Hassan Nasor Moyo tokea mwaka 1960 , nikiwa na umri wa miaka 17, pale alipokuwa akipigania haki za wafanya kazi wa znz, na kuongoza chama hicho cha Wafanyakazi wa znz, akishirikiana na Mzee Ahmed Hasan Diria.
Alikuwa akija Vikokotoni, nyumbani kwa Mzee Diria, mara kwa mara, kwa shughuli zao. Wakati wote huo, Zanzibar imekuwa ndio kiini cha misimamo yake, isiyotetereka, na yenye kutabirika. Hakupata kuwa mpinzani wa Muungano, si baada ya kuundwa, na wala si hii leo.
Mzee Moyo ndiye mtu pekee, aliye hai hii leo ambaye ameshuhudia binafsi utiaji saini wa Mkataba wa Muungano; hawezi kuwa mpinzani wa Muungano.
Anachopigania ni masilahi ya ZNZ tu, ndani ya Muungano.. Watu wanaweza kutofautiana naye katika mbinu na njia za kupata masilahi hayol, lakini kamwe hawezi kushutumiwa kuwa ni mpinzani wa Muungano. Kudai haki za Zanzibar si kupinga Muungano.
Bali, kuibeza na kuidharau Zanzibar ni kupinga Muungano; maana pasi na Zanzibar na "Tanganyika" hakuna muungano. Vivyo hivyo, kudai masilahi ya Tanganyika si kupinga muungano.
Hivyo, lazima watu waheshimu mawazo ya wengine katika kutetea kitu kimoja. Kumfukuza Mzee Moyo ni hasara kwa waliomfukuza na si kwa Mzee Moyo. Nimesikitishwa sana na kitendo hicho, ijapokuwa sikushangazwa. Ni kujikwaa kwa makusudi; unaoumia ni mguu siyo jiwe! Pitty! Pitty! Pitty!
Imeandikwa na: Balozi Abdulkadeer Shareef.
Imeandikwa na: Balozi Abdulkadeer Shareef.
Kusema kweli ni jambo la kusikitisha kumfukuza mzee kama huyu la kini inaonesha hawa walio mfukuza uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana
ReplyDeleteNaiunga mkono tafakuri ya Dk Abdulkeedir Shareef, kwa hakika ni jambo la kusikitisha kuona watu wenye misimamo tofauti na msimamo wa CCM Zanzibar wanadhihakiwa na kudhalilishwa huku ikisahaulika michango yao kwa Nchi yao ya Zanzibar, Mchango wa mzee Moyo hauna mithili kati ya waasisi wa nchi, ametumikia vyama vya wafanyakazi na kuwa ni miongoni mwa wajumbe wa Braza la Mapinduzi na Katibu wa mipango wa ASP, mzee Moyo ni muasisi wa CCM mwenye kadi nambari 7, inasikitisha leo eti kutoa maoni yake juu ya mfumo gani wa Muungano ni bora kwa wakati huu imekuwa ni kwenda kinyume na maadili ya CCM, wakati mchakato wa Katiba ukianzishwa kila mmoja alipewa fursa kutoa mawazo yake juu ya mfumo bora wa kuundeleza Muungano wetu, alichoambulia Mzee moyo ni dhihaka kutoka kwa watu ambao hawakuvuja hata tone la jasho lao katika ujenzi wa nchi hii, hii ni ishara ya kuanguka kwa CCM kwani fikra za kutaka mabadiliko juu ya hadhi ya Zanzibar katika Muungano zimeshastadi katika nyoyo za Wazanzibari, kamwe propaganda, chuki, dhihaka na visasi vya CCM havitoweza kuviza matumaini ya Wazanzibari kutaka haki yao katika muungano, Hongera mzee Moyo wewe ni shujaa wa Zanzibar.
ReplyDelete