Habari za Punde

Ziara ya Rais wa Zanzibar Kuwatembelea na Kuwafariji Wananchi Waliopata Maafa ya Mvua.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya kuwatembelea Wananchi wa Eneo la Kwahani kuwafariji kutokana na Mafaa za Masika zilizonyesha hjuzi na jana katika maeneo mbali ya Zanzibar na kuleta madhara makubwa. 
Afisa wa Idara ya Maafa Zanzibar akitowa Maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kuhusu jitihada waliochukuwa Idara yake kutowa huduma za Kijamii kwa Wananchi hao. wakati alipofika katika shehia ya kwahani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Sheha wa Shehia ya Kwahani Ndg. Nassir Ali Kombo, akitowa maelezo ya Wananchi wake waliofikwa na Maafa ya Mvua ya Masika ilionyesha juzi na kusababisha baadhi ya Wananchi wa eneo hilo kuhama nyumba zao kwa kujaa kwa maji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji Wananchi wa Kwahani wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuangalia athari za Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Wananchi wa Kwahani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipofika katika eneo hilo kuwafariji.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wazee wa Kwahani wakati wa ziara yake kutembelea maeneo yaliopata maafa kutokana na Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha Zanzibar katika maene mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dk. Halid , akimuonesha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, moja ya Nyumba zilizoharibiwa na Mvua inayomilikiwa na Ndg Omar Khamis Othman, Rais Shein, amefanya  ziara ya kuwafariji Wananchi waliopata Maafa hayo sehemu mbalimbali Zanzibar jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya kuwatembelea Wananchi waliopata maafa ya Mvua za Masika Zanzibar akiwa katika eneo la mwanakwerekwe akiendelea na ziara yake




Mkurugenzi wa Majenzi Eng Ramadhani Mussa, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kuhusiana na ujenzi katika eneo la bwawa la mwanakwerekwe, likiwa limefurika maji ya mvua na kuleta madhara kwa nyumba za jirani na bwawa hilo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Mkaazi wa Tomondo Bi Mwanakhamisi Takrima Mohammed, nyumba yake imekumbwa na maafa ya mvua za masika katika eneo hilo. Rais akiwa katika ziara yake kutembelea sehemu zilizoathiriwa ma Mvua Zanzibar.


Mwananchi wa Tomondo Ndg. Ali Khamis Khamis, akitowa maelezo, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipofika katika eneo la nyumba hiyo kuangalia maafa yaliosababishwa na mvua zinazonyesha katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.




Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa wanaoishi maeneo ya  ziwa mabonga alipofika katika eneo hilo kuwafariji Wananchi waliopata maafa ya kuharibika kwa nyumba zao kutokana na mvua za masika

1 comment:

  1. ukiingalia picha ya wananchi kwa kina, utaona wamekata tamaa na kinachofanyika hapo ni porojo za siasa. Kwani hamkujua mvua zinaweza kubwa na kuweza kuleta maafa. Kwa nini mitaro isingesafishwa, mabwawa yakachimbuliwa, na waliojenga kwenye njia za maji wakabomolewa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Barabara ya mwanakwerekwe mainjinia waliohusika wasimamishwe na Waziri lazima ajiuzulu. Tumechoka na blaa blaa na siasa zenu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.