Msajili wa Hazina, Lawrence
Mafuru (katikati), akikata tepe kikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za
kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9,
2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto
ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi YA tpb, Profesa Lettice Rutashobya
Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki katika tawi la Babati, mkoaniManyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Prof. Lettice Rutashobya.
Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA, Babati
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake
jipya kwenye mji wa Babati mkoani Manyara. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari
9, 2016, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema
tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji
wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.
‘’Tawi
hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za
kibenki karibu zaidi na wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na
za kisasa ikiwemo ile ya ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa
ujumla katika wilaya hii ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.
Profesa
Rutashobya aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake
kwa kutumia huduma wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia
huduma za Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya
matawi yanayofanya vizuri kifaida.
Naye
Msajili wa Hazina, Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za
kibenki za tawi hilo, aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya
kuninua maisha ya Mtanzania ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki
karibu na jamii hiyo, na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye
lengo la kumuinua kimapata mwananchi wa chini.
Msajili
huyo wa Hazina, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia
fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba
mikopo ambayo oinatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.
Kwa
upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi amesema
uamuzi wa kujenga tawi hilo ambalo linatoa huduma zote zinapatikana kwenye
matawi mengine ya Benki ya Posta Tanzania nchi nzima.
“Azma
ya Benki ya Posta, ni kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote
(financial Inclusion), alisema Moshingi.
<!--[if gte mso 9]>
No comments:
Post a Comment