Habari za Punde

Tamko la Viongozi wa dini wa Bara na Visiwani



UTANGULIZI:

Kufuatia hali ya Amani Zanzibar kuwa mashakani kutokana na mgawanyiko miongoni mwa jamii unaosababishwa na tofauti mbalimbali zikiwemo za kisiasa. 

Baraza la Viongozi wa Dini mbalimbali kwa Ujenzi wa Amani Tanzania (IRCPT) wamewakutanisha viongozi wa Dini wa madhehebu mbalimbali ya Ukristo na Uislam na Jumuiya ya Hindu kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuzungumzia hali halisi Zanzibar na nini kifanyike kudumisha amani, ambao baada ya majadiliano ya kina wameazimia yafuatayo:

MAAZIMIO:
Kwakutambua kuwa Zanzibar ni moja na watu wake ni wamoja na amani ni tunu adhimu kwa watanzania wote,

1. Viongozi wa Dini tunawapongeza Watanzania wenzetu wa Zanzibar kwa kuwa wavumilivu na kuilinda Amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi hadi sasa.
2. Viongozi wa Dini, wajitenge na siasa za vyama, kwani wao wanapaswa kua nguzo za jamii zenye Imani na asili tofauti, wasuluhishi na watetezi wa Amani nchini
3. Vyomba vya usalama, wawabaini na kuwachukulia hatua vikundi vya uvunjifu wa Amani ili wananchi waishi kwa Amani. (Watumie nguvu inayostahili na isiogopesha umma)

4. Vyama vya siasa vinavyotoa kauli nataarifa zisizo sahihi na kuleta uchochezi. Viache muenendo huo ili kudumisha Amani. Kwani kila mmoja anawajibu wakuiteteaTunu hii yaTaifa.
5. Tume ya Uchaguzi, wawe waadilifu, kusimamia haki, sheria, kanuni na uwazi ili kudumisha Amani katika kipindi hiki cha uchaguzi
6. Vyombo vya habari visaidie kuhakikisha tunapita kwenye uchaguzi kwa usalama na amani kwa kutoa taarifa sahihi, kuzingatia maadili na kufuata taratibu na sheria zilizopo.
7. Mahali ambapo uvunjifu wa Amani na wahusika ni dhahiri vyombo vya usalama wachukuliwe hatua stahiki za kisheria.
8.  Wananchi ambao pia ni waumini wetu wailinde Amani kutoka mioyoni mwao, kwani ni wajibu wao wa kiroho na kijamii.
9. Wananchi watakaoshiriki kupiga kura wakitumia haki yao ya kimsingi, wahakikishiwe Amani na wale ambao hawatashiriki wasibugudhiwe na wao pia wahakikishiwe Amani.
“ZANZIBAR MOJA, WATU WAKE NI WAMOJA, TUUNGANE KULINDA AMANI KWA MAENDELEO YETU”
“AMANI KWANZA”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.