Habari za Punde

JKU waanza vibaya Kombe la Shirikisho yafungwa 4-0 na Sport Villa ya UgandaMike Ndera akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya JKU katika uwanja wa Namboole , Uganda


JKU  ya Zanzibar imefungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Mandela, Kampala, na wenyeji SC Villa ya Uganda. 


Mabao ya Jogoo Jogoo la Kampala yamefungwa na Mike Ndera, Mike Serumaga, Umar Kasumba na Godfrey Lwesibawa. Sasa JKU ) itabidi ishinde 5-0 wiki ijayo Uwanja wa Amaan, Zanzibar ili kusonga mbele.

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Azam FC wanashuka Uwanja wa Bidvest mjini Johannesbrug, Afrika Kusini kumenyana na wenyeji Bidvest Wits katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza.

Yanga timu pekee iliyobaki Ligi ya Mabingwa, imeanza vizuri kwa ushindi wa 2-1 ugenini dhdi ya wenyeji APR Uwanja wa Amahoro, Kigali

1 comment:

  1. JKU na mpira? wache wakatese watu ovyo ovyo huko.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.