Habari za Punde

Balozi Seif apokea msaada wa dawa, akagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko

 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi msaada wa Dawa na Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo kwa ajili ya wananchi walioathirika na maradhi ya kipindu pindu.

 Balozi Seif akipokea msaada wa vifaa kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora Ofgisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

 Hali halisi ya Bara bara iliyotoka Amani chini kuelekea kwa wazee welezo ambayo imebomoka vibaya kutokana na kasi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka maeneo ya welezo juu.

 Baadhi ya Nyumba mbali mbali zilizojaa maji kufuatia mafuriko ya kuamkia Jumapili iliyopita katika Mtaa wa Kara kana Chumbuni Mjini Zanzibar.

 Balozi Seif akiwa na Uongozi wa Wilaya ya Magharibi zote mbili “A” na “ B” akikagua Bara bara itokayo Kwerekwe kuelekea Fuoni Makaburini ambayo imefunikwa na maji kufuatia mvua za juzi usiku.

 Bara bara ya Kwerekwe kuelekea Fuoni ikionekana kama shamba lililotelekezwa kutokana na kufukiwa na majani ya mayungi yungi yaliyokokotwa na maji na kupiga kambi kati kati ya bara bara hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwapungia Mkono Wananchi wa maeneo mbali mbali waliohifadhiwa katika Skuli ya Sekondari ya mwanakwerekwe baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko juzi usiku.
Hali halisi ya eneo la Ziwa Maboga liliopo Kijiji cha Kisauni ambalo maji yake yamefurika hadi katika makaazi ya wananchi wa eneo hilo waliojenga pembezoni mwa ziwa hilo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

1 comment:

  1. muandishi wacha kuchagua comments za kuonesha, mtu anakosowa tu, hamna matusi wala nini, kama mumekosea ni vizuri mukumbushwe sasa vumilia tu muandishi, japo inauma lakini stahmili

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.