Habari za Punde

Baraza la Tiba asili na tiba mbadala Zanzibar lafanya ziara ya kushtukiza kliniki na Maduka ya dawa asili

 Mmiliki wa kliniki ya ‘Madawa Herbal Clinic’ ya Bububu Kijichi Muh’d Said Ali akitoa maelezo kuhusu huduma anazotoa  katika kliniki yake baada ya wajumbe kutoka  Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kufika katika kliniki yake  kufuatilia shutma za kulaza wagonjwa  kitu ambacho kinakatazwa, wa mwanzo (kulia) Mrajis wa Tiba asili Zanzibar Haji Juma Kundi.
Mrajis wa Tiba asili Zanzibar Haji Juma Kundi akitembelea  maduka mbali mbali  ya kuuzia  dawa za asili wakiwa kwenye ukaguzi wa kawaida kuangalia ubora wa dawa na hati za usajili wa maduka hayo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.