Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Atembelea Kambi ya Wananchi Waliopata Maafa ya Mvua Skuli ya Mwanakwerekwe C Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,, akitembelea na kuwafariji Wananchi Wananchi waliopata Maafa ya Mvua za Masika hivi karibu nyumba zao kujaa maji na kukosa hifadhi na kuhifadhiwa katika Kambi hiyo ilioandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ajili yao na kupa misaada yote ya Kijamii akiwa na Mkuu wa Kambi hiyo Bi Rahma Kassim Ali, wakati wa ziara yake hiyo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkuu wa Kambi ya Wananchi waliopata Maafa ya Mvua Bi Rahma Kassim Ali, wakati alipofika katika kambi hiyo kuwafariji na kuwapa pole Wananchi hao.kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe Issa Haji Ussi Gavu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Ndg Ali Juma Hamad akitowa maelezo kwa Rais kuhusiana na misaada ya Kijamii wanayotowa kwa Wananchi hao wakiwa katika Kambi hiyo ya Skuli ya Mwanakwerekwe C, Zanzibar. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Shein wakati wa ziara yake kuwatembelea Wananchi waliopata maafa ya mvua kujaa maji kwa nyumba zao na kuhifadhiwa katika kambi hiyo ilioko Skuli ya Mwanakwerekwe C Zanzibar. 
Baadhi ya Watoto wanaoishi katika Kambi hiyo kwa muda wa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipofika kuwatembelea na kuwafariji kutokana na maafa hayo ya Mvua za masika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Wananchi waliopata maafa ya kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar Dk Shein, kuzungumza na Wananchi hayo na kuwafariji na mkasa huo wa kuingiliwa na maji ya mvua katika makaazi yao.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi waliopata maafa ya Mvua za Masika kwa kuingiliwa na maji katika nyumba zao na kuhifadhiwa katika Kambi hiyo Skuli ya Mwanakwerekwe C, na kupatiwa mahitaji yote ya Kijamii muda wanaokuweko katika Kambi hiyo. 
 Wananchi wanaoishi katika Kambi ya muda Skuli ya Mwanakwerekwe C baada ya nyumba zao kuingia maji wakati wa mvua za masika zikinyesha hivi karibu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia na kuwapa pole kwa mkasa huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijumuika na Viongozi wa Serikali na Wananchi wakiitikia dua baada ya kumaliza ziara yake katika Kambi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mji Mhe Abdi Mahmoud akisoma dua baada ya kumalizika kwa ziara ya Rais wa Zanzibar Dk Shein, kuwatembelea Wananchi waliopata maafa wakiwa katika Skuli ya Mwanakwerekwe C Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiondoka katika Kambi ya  Wananchi Waliopata Maafa katika Skuli ya Mwanakwerekwe Zanzibar akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed.baada ya kumaliza ziara yake kuwatembelea Wananchi hao na kuwapa pole kwa mkasa huo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.