Habari za Punde

Kampeni ya Tokomeza Kipindupindu jimbo la Kikwajuni

KAMPENI YA TOKOMEZA KIPINDUPINDU NA SAFISHA JIMBO LA KIKWAJUNI.

Mhe. Mbunge, Mwakilishi na Madiwani wa Jimbo la Kikwajuni wanawatangazia wananchi wote kushiriki katika kampeni maalum ya kufanya usafi Jimbo la Kikwajuni kwa kuanzia na Shehia ya Kisimamajongoo na Kikwajuni Bondeni, itakayoanzia Kisimamajongoo nyuma ya kituo cha Polisi siku ya Jumapili, tarehe 24/04/2016 saa 2 kamili asubuhi, pamoja na uzinduzi wa Kikundi cha Usafi wa Mazingira utakaofanyika siku hiyo hiyo na pahala hapo hapo jioni yake saa 10 kamili jioni, ambapo pia kutakua na Mkutano wa Shukurani wa wananchi wote. 

Shime wananchi jitokezeni kwa wingi na kila mwenye kifaa cha kufanyia usafi aje nacho ili tutokomeze kwa pamoja maradhi thakili ya Kipindupindu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.