Habari za Punde

Chuo cha Kuhifadhi Qur-an Kujengwa Kisiwani Pemba

Jumuiya kimataifa ya International Holly of Quran Memorazation yenye makao yake nchini Saudi Arabia inatarajia kufungua chuo cha kuhifadhia Qurani Kisiwani Pemba hivi karibuni ilikuendeleza watoto wakislamu kujifunza kuhifadhi qurani  kwa wingi visiwani humo..

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Kisiwani Pemba Mjumbe wa tasisi hiyo Abdul Azizi al-Umiry amesema madrasa hiyo  tayari imeanza kujengwa  na inatarajia kumalizika hivi karibuni

Amesema ujio wao kisiwani pemba ni kutoa mafunzo kwa walimu wa madrasa na wanafunzi walio kwisha hifadhi Quran juzuu 30 ili kutafuta mbinu bora za kuwafundisha wanafunzi njia itakayo kuwa nyepesi kwao kuhifadhi kitabu kitukufu cha Qur an

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzio hayo mbunge wajimbo la Mgogoni DR Suleiman Ali Yusufu amesema ujio wa huo ujumbe ni jitihada zinazo endelea kufanywa na jumuiya ya kuhifadhi Quran kisiwani humo ili kufanikisha maendekleo ya kuhifahi qurani kisiwani pemba

Ujumbe huo unatarajiwa kuwepo Pemba kwa siku mbili na utaendelea na mafunzo kama hayo huko Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.