Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani Yaadhimishwa Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.


Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza MC akitowa maelezo ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimishwa katika Ukumbin wa Jumba la Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr akisoma risala ya wakunga katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) akitoa salamu za Shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed akionyesha vitabu viwili vya maadili ya wakunga na wauguzi alivyovizindua katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed akihutubia Wakunga walioshiriki maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Wageni waalikwa wakiwa katika ukumbi wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimishwa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mwakilishi wa Jumuia ya CHARA (katikati) akiongoza kukata Keki ya maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.