Na MwandishiMaalum, New York
Umoja wa Mataifa,
jana Mei 19 umefanya hafla maalumu ya siku ya Kimataifa ya Walinzi wa
Amani
wanaohudumu katika Misheni mbalimbali za Kulinda Amani
chini ya kofia ya Umoja wa Mataifa.
Katika hafla hiyo jumla ya walinzi 129 wanajeshi na polisi waliopoteza maisha mwaka jana kwa kushambuliwa na makundi ya wapiganaji wenye silaha,
matukio ya kigaidi, ajali na kuumwa walikumbukwa na kuenziwa kwa mchango wao.
Miongoni mwa Mashujaa hao 129 kutoka nchi
50, wapo mashujaa watatu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mashujaa hao ni
Sgt. Musa Abdrahamani Yusuf, Cpl. John Leornad Mkudena Pte.Juma Ally
Khamis.
Hafla hiyo maalum ya kutambua mchango wa walinzi hao wa
Amani
na ambao wamejitolea maisha yao kwa ajili ya kuwalinda na kuokoa maisha ya wananchi wasio kuwa na hatia katika nchi zinazokabiliwa na
vita na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe iliongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki
Moon.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, ndiye aliyepokea medali maalum za mashuja hao watatu kwa niaba ya familia zao.
Medali waliyotunukiwa mashujaa hao na wengine inatambuliwa kama medali ya Dag Hammarskjold.
Hafla ya mwaka huu,
pamoja na kutambua mchango wa mashujaa hao 129 , pia
ilitambua kwa namna yapekee na kwa mara ya kwanza, mchango na kujitolea wa hali ya juu ulikofanywa na Kapteni Mbaye Diagneraiaya Senegal,aliyepoteza maisha mwaka 1994 wakati akiokoa maisha ya wanyarwada wakati wa mauaji ya kimbali.
Kapteni Mbaye Diagne ameeziwa rasmi katika maadhimisho ya mwaka huu kwa kupewa medali maalum iliyopewa jina
la Medali ya Mbaye Diagne, medali ambayo alikabidhiwa mjane wa Mbaye
Bibi Yacine Mar Diophuku akishuhudiwa na watoto wake wawili.
Kapten Mbaye Diagne alikuwa mwangalizi wa Amani nchini
Rwanda, kwa ushujaa mkubwa na bila ya kujali hatariiliyokuwaikimkabilialitumialorikuwafichanakuwapelekamahalisalamamamiayawanyarwadawakatiwamauajiyakimbaliya
Rwanda.
Kwa kutambuaushujaanauthubutu wake huo, Baraza la
Usalamalilibunimwaka 2014
medaliyaKaptenMbayeDiagneambayowatakuwawanatunukiwawanajeshi, polisinaraiaambaowameonyeshauthubutunaushupavuwahaliyajuukiasi
cha kupotezamaishayaowakatiwakitekelezamajukumuyao.
Akizungumzawakatiwahalfahiyoambayoilibebamajonziyaainayake, KatibuMkuuwaUmojawaMataifa, Ban Ki Moon, alielezakwamba, hadikufikiamweziwannemwakahuu,
jumlayawalinziwa Amani 3,400
wakiwamowanajeshi, polisinaraiawalikuwawamepotezamaishatangukuanzishwawashughulizaulinziwa
Amani kwakofiayaUmojawaMataifamiaka 70 iliyopita.
“Wakatileotunawaenzinakuwakumbukamashujaahawa 129
kutokamataifa 50 waliopotezamaishayaomwakajanawakatiwakitekelezajukumu la
kuwalindawananchiwengine, jana ( Mei 18)
walinziwenginewatanowanaohudumuhuko
Mali
wamepotezamaishabaadayakushambuliwa”. AkasemaBan Ki Moon kwahuzuni.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akiwa ameshika medali ya Dag Hammarskjold waliyotunukiwa mashujaa watatu watanzania ambao wamepoteza maisha mwaka jana wakati wakihudumu katika Misheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. kushoto kwa Balozi ni Luteni Kanal George Ita'ngare, mshauri wa masuala ya kijeshi katika Uwakilishi wa Kudumu na kulia ni Bw,Herve Ladsous, Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinsi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akimvisha Bibi Yacine Mar Diop medal maalum ya Kapteni Mbaye Diagne ambaye alikuwa ni mume wa Bibi Yacine, Kapteni Diagne aliuawa mwaka 1994 wakati wa mauaji ya kimbali ya Rwanda. medali hiyo maalum imebuniwa na Baraza la Usalama kwa kutambua ushujaa na uthubutu wake na kujituma kwake kwa hali ya juu hadi kupelekea kupoteza maisha. Kapteni Diagne anakumbukwa kwa namna alivyookoa maisha ya mamia ya wanyarwanda kwa kuwaficha kwenye lori na kuwapeleka mahali salama kabla ya yenye mwenyewe kuuawa
Balozi Tuvako Manongi akiandika katika kitabu cha kuwaeni walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa waliopotea maisha mwaka jana. miongoni mwa mashujaa 129 waliokumbukwa wapo watanzania watatu ambao ni Sgt. Musa Abdrahamani Yusuf, Cpl John Leornad Mkude na Pte. Juma Ally Khamis
Sehemu ya washiriki wa hafla ya siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa hafla hiyo ilifanyika jana Mei 19
No comments:
Post a Comment