Habari za Punde

Uzinduzi wa Tamasha la Michezo la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar Kuzinduliwa Kesho katika Uwanja wa Amaan Zanzibar

Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar Ndg.Abdulatif Kadir Mussa, akizungumza na Waandishi wa habari za michezo Zanzibar kuhusiana na Tamasha la Michezo la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu linalotarajiwa kuzinduliwa kesho katika Uwanja wa Amaan Zanzibar na kushirikisha Vyuo 16 vya Zanzibar kwa Michezo ya Mpira wa Miguu, Netiboli, Kufuta Kamba na michezo mengine,. Tamasha hilo likiwa na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni
Mazingira Safi na Salama, Shiriki Michezo kwa Afya Yako na Elimu Bora Kwa Maisha      
Mwenyekiti Kamati ya Michezo ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar Ndg Rashid Muhidin Mohammed, akizungumzia maandalizi ya Tamasha hilo la Michezo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya michezo Zanzibar. 
 Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Viongozi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Elimu ya Zanzibar kuhusiana na Uzinduzi wa Tamasha la Vyuo Vikuu Zanzibar kesho.
 Katibu wa Shirikisho la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar Juma Omar akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kukamilika kwa Tamasha la Michezo la Vyuo Vikuu Zanzibar linalotarajiwa kuzinduliwa kesho katika viwanja vya Amaan Zanzibar na kushirikisha Michezo mbalimbali itakayochezwa na Wanafunzi wa Vyuo,Vikuu Zanzibar 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.