Habari za Punde

Salamu za Rambirambi kwa Kifo cha Balozi Mdogo wa Oman Aliyekuwa Zanzibar.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                                    20.05.2016

---
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, amemtumia salamu za rambi rambi Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nje wa Oman Mhe. Yusuf bin Alawi bin Abdullah kufutia kifo cha Balozi mdogo wa Oman aliyopo Zanzibar Mhe. Ali Abdallah Al-Rashid.

Katika salamu hizo za rambi rambi, Waziri Gavu alisema kuwa amepokea kwa  masikitiko na mshituko mkubwa taarifa ya kifo cha  Balozi Ali Abdallah Al-Rashid kilichotokea hivi karibuni hapa Zanzibar.

Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wote wa Zanzibar, alitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na wananchi wote wa Oman kufuatia msiba huo mkubwa.

Aidha, salamu hizo za rambirambi zilieleza kuwa Wazanzibari watamkumbuka sana Balozi Ali Abdalla Al-Rashid kwa juhudi zake za kuuendeleza na kuuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Oman.

“Nakuhakikishia Mhe. Waziri kwamba sote tupo pamoja na wanafamilia pamoja na wananchi wote wa Oman katika kipindi hiki kigumu cha msiba”, zilieleza salamu hizo.

Pamoja na hayo, salamu hizo zilimuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu Balozi Ali Abdalla Al-Rashid mahali pema peponi. Amin.

Balozi Ali Abdallah Al-Rashid alifariki dunia katika hospitali ya Global  hapa Zanzibar baada ya kukabiliwa na shindikizo la damu na baada ya kifo chake mwili wake ulisafirishwa kuelekea nchini Oman kwa ajili ya mazishi.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.