Habari za Punde

Mhe Mapunda Akabidhi Rasmin Mikoba ya UVCCM Kwa Kaimu Katibu Mkuu Ndg Shaka Hamdu Shaka Dar.

Leo tarehe 20 May 2016 saa saba kamili mchana.aliekuwa katibu mkuu wa UVCCM Mh Sixtus Mapunda ambae kwa sasa Ni Mbunge wa Mbinga Mjini amekabidhi rasmi ofisi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM ndugu Shaka Hamdu Shaka ambae alikiwa naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar.


Kutokana na kubanwa na Majukumu ya Ubunge na kuongeza ufanisi wa ofisi ya Vijana Mh Sixtus Mapunda amekabidhi ofisi  rasmi Ili kutoa nafasi zaidi kwa Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Shaka Kusimamia ofisi vizuri zaidi.Umoja wa vijana unatoa Pongezi na shukurani kwa Mh Sixtus Kwa utumishi wake wote ndani ya UVCCM na tunamtakia kila la kheri Katika utumishi wake mpya kama mbunge wa mkoa wa Ruvuma.
Aliitumikia CCM na UVCCM kwa dhati na muda mrefu hadi sasa amekuwa Mbunge wa CCM ni imani yetu kuwa ataendelea kuwa karibu wakati wote kwa Maslahi ya CCMTunawaomba  Vijana wa CCM na Watanzania wote nchi nzima kumpa ushirikiano wa kutosha Kaimu katibu Mkuu ndugu Shaka Hamdu ili kuiendeleza jumuiya yetu Mbele zaidi kwa Maslahi ya Chama na nchi yetu.Imetolewa na :
ABUBAKAR D. ASENGA
KAIMU MKUU WA IDARA Hamasa, Sera,utafiti na mawasiliano 
UVCCM MAKAO MAKUU

NB:
UVCCM inaendelea kuuomba umma kuendelea kupuuza taarifa zote za uzushi zinazosambazwa kuhusu UVCCM na baadhi ya vijana wa vyama pinzani wakitafuta Pakutokea baada ya kubanwa na kasi ya Rais Magufuli

HATUTARUDI NYUMA KWENYE KUTUMBUA MAJIPU
KILA ANAEKUMBATIA JIPU ATAKUWA  NA Harufu ya Usaha.

HAPA KAZI TU
SIMU 0627968722.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.