TANGAZO
TRA ZANZIBAR INAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE WA
UNGUJA NA PEMBA, KWAMBA TAREHE YA MWISHO YA KULIPIA AWAMU
YA TATU YA KODI YA MAPATO YAANI INCOME TAX NI TAREHE 30
SEPTEMBA 2016.
MALIPO YA KODI YATAKAYOLIPWA BAADA YA TAREHE 30
SEPTEMBA 2016 YATALIPWA PAMOJA NA ADHABU YA KUCHELEWESHA
MALIPO.
AIDHA WAFANYABIASHARA WANAKUMBUSHWA KWAMBA, TAREHE YA
MWISHO YA KUWASILISHA RITANI ZA MWISHO ZA KODI YA MAPATO
(INCOME TAX) KWA MWAKA WA MAPATO UNAOISHIA TAREHE 31 MACHI
2016 NI TAREHE 30 SEPTEMBA 2016.
TUNAWAOMBA WAFANYABIASHARA WOTE WAZINGATIE MUDA WA
KULIPA KODI NA KUWASILISHA RITANI ZA MWAKA, ILI KUEPUKA KULIPIA
KODI ITAKAYOAMBATANA NA ADHABU.
KWA UFAFANUZI ZAIDI UNAWEZA KUFIKA KATIKA OFISI ZA MAMLAKA
YA MAPATO TANZANIA (TRA) ZILIZOPO MAYUGWANI KWA UNGUJA NA
KILIMATINDE CHAKECHAKE KWA PEMBA,
‘‘PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU’’
Imetolewa na:
Kitengo cha Elimu na Huduma kwa Mlipakodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania-Zanzibar
Simu nambari 0242232923
S. L. B. 161 ZANZIBAR
Barua pepe: trazanzibar@tra.go.tz
No comments:
Post a Comment