Habari za Punde

Dhifa ya Chakula cha Usiki Kilichoandaliwa kwa Wageni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Rais wa Zambia Edga Lungu,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa Rais wa Zambia jana,katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.28-11-2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta na Rais wa Zambia Edga Lungu wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika  hafla ya  chakula cha jioni aliyoiandaa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa Rais wa Zambia Edga Lungu katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Zambia Edga Lungu akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini  kwa ziara ya siku tatu
Rais wa Zambia Edga Lungu akisalimiana na Makamo wa Rais Mstaafu wa   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati wa hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini  kwa ziara ya siku tatu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe  Magufuli akifuatana na Rais wa Zambia Edga Lungu baada ya kumalizika hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,Rais Lungu yupo nchini  kwa ziara ya siku tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiagana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kumalizika hafla ya dhifa ya chakula cha jioni iliyofanyika jana katika ukumbi wa ikulu ya Jijini Dar es Salaam,iliyoandaliwa kwa Rais wa Zambia Edga Lungu akiwa nchini kwa ziara ya siku tatu, [Picha na Ikulu.]28/11/2016.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.