Kamishina wa Sera kutoka Wizara ya Fedha,
Mipango na Uchumi Bw. Augustine K. Ollal akizungumza wakati wa ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa Tatu wa Wawakilishi wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha
Hazina (Hazina Saccos) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Chama hicho Bw. Eligius A. Mwankenja.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama
cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Hazina (Hazina Saccos) wakifuatilia
Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Chama cha Ushirika cha Akiba
na Mikopo cha Hazina (Hazina Saccos) Bw. Eligius A. Mwankenja (wa kwanza
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Hazina Saccos leo
jijini Dar es Salaam. Watatu kutoka kushoto mstari wa mbele ni Mwenyekiti wa
Bodi hiyo Bw. Eligius A. Mwankenja.(Picha
na: Maelezo)
Na: Frank Shija –
Maelezo.
CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina
Saccos kimepanga kujenga kitega uchumi cha kisasa kupitia mradi wa njedengwa katika
Mkoa wa Dodoma ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia
makao makuu ya shughuli za Serikali
mjini humo.
Hayo
yamebainishwa na leo Jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Eligius Mwankenja wakati wa mkutano Mkuu wa
mwaka wa Chama hicho, na kuongeza kuwa mradi huo katika hatua ya utafiti wa
kiuchumi na fedha.
Mwankenja amesema
kuwa wapo katika hatua za awali za kuanza utekelezaji wa mradi huo ambao zabuni
yake inatarajiwa kutangazwa mwezi wa Aprili 2017.
“Mradi wa Njedengwa
upo mbioni kuanza tunategemea utakuwa chachu ya maendeleo ya Chama chetu kwa
kutuingizia kipato kutokana na shuguli zitakazokuwa zikifanyika kupitia mradi
huo”. Alisema Mwankenja.
Aliongeza kuwa
kupitia mradi huo wanatarajia kujenga hoteli ya kisasa, kumbi za kufanyia
mikutano, majengo la Ofisi, , Viwanja vya Michezo na bwawa maalum la kuogelea.
Mpaka sasa tayari
upembuzi yakinifu wa hali ya eneo hilo imekwishafanyika ambapo mradi huo
utajengwa kwa ubia baina ya mwekezaji kupitia utaratibu wa Jenga, Endesha na
Hamisha (Build, Operate and Transfer - BOT) ambapo mwekezaji atagharamia ujenzi
wote na kuendesha kwa muda ambao utakualiwa ndani ya mkataba.
Palimo na mafanikio
hakukosi kuwa na chamagamoto, Mwenyekiti wa Bodi ya Hazina Saccos anasema kuwa
changamoto kubwa wanayokumbana nayo kwa sasa ni ufinyi wa ofisi ukizingatia
kwamba idadi ya wananchama imeendelea kuongezeka toka wanachama 100 mwaka 1972
wakati Hazina Saccos ilipoanzishwa hadi kufikia zaidi ya 5000 mwaka huu.
Changamoto hii
inasababisha pia kuongezeka kwa mahitaji ya wanachama wanaohitaji kupatiwa
mikopo, hivyo inakilazimu chama kubuni njia mbada za kukuza na kuongeza mtaji
ili kukabiliana na hali hiyo.
Mradi wa Njedengwa ni
mradi wa uwekezaji wa Hazina Saccos katika kuhakikisha wanawekaza ili kukuza
mtaji wa Chama chao kwa lengo la kuhakikisha kinawahudumia wanachama wake wote
i kulingana na mahitaji yao kwa wakati.
No comments:
Post a Comment