Habari za Punde

Skuli ya maandalizi ya Highlight yakabidhi vyeti kwa wanafunzi waliomaliza muda wao

 Wanafunzi wa Nasari ya Highlight ilioko Wawi Pemba, wakisoma Duwa maalumu kabla ya mkuu wa Wilaya kuhutubia wananchi katika mahafali ya mwanzo ya Nursery hiyo.
 Wanafunzi wa Nasari ya Highlight iliopo Wawi, Wakiimba Wimbo maalumu wa Skuli hiyo kabla ya mgeni rasmi ambae pia  Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake , Salama Mbarouk Khatib, kuzungumza na hadhara na kukabidhi
vyeti kwa wanafunzi waliomaliza muda wa kusoma Nursery

 Jengo la Nursery ya Highlight , lilopo katika kijiji cha Wawi Pemba, ambayo nia yake nikuwa Nursery na Primary.
 Wanafunzi  wa Nursery ya Highlight iliopo Wawi Pemba, wakionesha michezo mbali mbali kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba , Salama Mbarouk Khatib.

 Mwalimu mkuu wa Nursery ya Highlight, akitowa Maelezo kwa mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba,Salama Mbarouk Khatib, huko Wawi Pemba..
 Mkurugenzi wa Skuli ya Nasari ya Highlight , Hamad Bakar Ali, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kukabidhi vyeti kwa wanafunzi wanaomaliza muda wa kusoma Nursery

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib, akizungumza na Wananchi wa Wawi , juu ya umhimu wa kuwapeleka watoto wao Skuli hiyo ya Nursery na kupambana na udhalilishaji wa Watoto, katika mahafali ya mwanzo ya skuli hiyo

 Wanafunzi wa Nasari hiyo , wakimskiliza Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, akitowa nasaha kwa Wazazi wa watoto hao huko Wawi Pemba.

Picha ya pamoja katika ya Wanafunzi wa Skuli ya Nasari ya Highlight ya Wawi Chake Chake na Mkuu wa Wilaya hiyo huko Skulimi kwao Wawi -Pemba.


 Picha na Bakar Mussa -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.