Habari za Punde

Jang'ombe Boys yapata shavu kucheza Sportpesa Super up

 WATASHINDANA NA KINA YANGA, SIMBA, SINGIDA UNITED, GOR MAHIA, NAKURU ALL STAR NA LEOPARD

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya Soka ya Jang’ombe Boys inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imepata bahati ya kuwemo kwenye Mashindano ya  Sport Pesa Cup yanayotarajiwa kuanza kutimu vumbi June 5, 2017 jijini Dar es salam.

Ligi hiyo itashirikisha jumla ya timu 8 kutoka Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili.

“Ni kweli kwa hapa Zanzibar Jang’ombe Boys pekee wamepata mualiko kucheza Ligi hiyo ambayo itahusisha vilabu vikubwa vya Bara na Kenya”. Kilieleza chanzo.
RATIBA KAMILI HIYO
5/6/2017
Singida united Vs FC leopard
Yanga Vs Tusker fc
6/6/2017
Simba Vs Nakuru All Star
Jang`ombe boys vs Gor mahia
Nusu fainali tarehe 8/6/2017
Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard atacheza na bingwa kati ya Yanga na Tusker.

Nusu fainali ya pili Bingwa wa mechi kati ya Simba na Nakuru all-star atacheza na bingwa wa mechi kati ya Jangombe boyz na Gor mahia

Fainali ni tarehe 11/6/2017 ambapo Bingwa wa SportPesa Super Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.