Habari za Punde

Kundemba FC yaibuka kidedea mashindano ya Masauni - Jazeera Cup

 Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Kundemba FC,Mohamed Haji Shaibu, baada ya kuibuka mshindi katika  mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Visiwani Zanzibar. Picha na Abubakari Akida
 Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi zawadi ya viatu  mchezaji bora wa mashindano ya Masauni - Jazeerah Cup,Shabani Makuka.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka mshindi  dhidi ya Kilimani Maghorofani, mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja,Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida
 Nahodha wa timu ya Kundemba FC, Mohamed Haji Shaibu, akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza  wa mashindano ya Masauni-Jazeera Cup  kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt.Abdulla Juma Saadala.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni .Picha na Abubakari Akida
 Nahodha wa timu ya Kundemba FC,Mohamed Haji Shaibu, akifurahia  fedha za  zawadi ya mshindi wa kwanza mashindano ya Masauni-Jazeera  baada ya kuzipokea  kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala,(aliyeshika kombe).Picha na Abubakari Akida

 Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akizungumza na wananchi (hawapo pichani), waliofika kuangalia mchezo wa fainali wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani,uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja, Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Kundemba FC, wakishangilia kuibuka mabingwa wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup, baada ya kuifunga timu ya Kilimani Maghorofani kwa ushindi wa mikwaju ya penati 8-7.Mchezo huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.