TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampuni ya Rafiki Network inawaarifu kwamba itafanya Tamasha la
Michezo na Utamaduni linalojulikana kama“ Pemba
Weekend Bonanza” litakalofanyika kisiwani Pemba kuanzia tarehe 28 hadi 30 Julai mwaka 2017.
Tamasha hilo litajumuisha matukio mbali mbali kama
vile mchezo wa ng’ombe, resi za baiskeli, mashindano ya kuogelea na resi za ngalawa.
Mchezo wa ng’ombe utafanyika siku ya Ijumaa tarehe
28 Julai, 2017, majira ya lasiri katika viwanja vya skuli ya Chwale, Wilaya ya Wete,
Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aidha,
resi za baiskeli ambazo zitafanyika kwa mizunguko mwili tafauti zitakuwa siku ya Jumamosi tarehe
29 na Jumapili tarehe 30 Julai katika maeneo na utaratibu ufuatao:
Siku ya Jumamosi, tarehe 29 Julai,
resi za baiskeli hatua ya mchujo, zitafanyika kwa kujumuisha makundi matatu yanayokimbia kwa kupitia barabara tatu tafauti kiswani
Pemba kama ifuatavyo:
- Resi za Baisikeli kutoka Mkoani hadi Uwanja wa Gombani
(Stadium) Chake Chake Pemba
- Resi za Baisikeli kutoka Gando hadi Uwanja wa Gombani
(Stadium) Chake Chake Pemba.
- Resi za Baisikeli kutoka Konde hadi Uwanja wa Gombani
(Stadium) Chake Chake Pemba.
Washindi
10 kutoka kila kikundi na barabara zilizotajwa hapo juu wataingia katika hatua ya fainali za resi za baiskeli zitakazofanyika siku ya Jumapili kama ilivyotajwa hapo awali.
Fainali za resi za basikeli zitaanzia Uwanja wa Gombani hadi Vumawimbi, Makangale Pemba
majira ya saa 1 kamili asubuhi.
Kwa
upande mwengine,
kutakuwa na mashindano ya kuogelea baharini yatakayofanyika siku ya Jumapili, Tarehe 30
Julai 2017 katika fukwe za Vumamwimbi.
Shindano hili litawashirikisha waogeleaji mbali mbali nchini ambao washiriki wapatao 100
watachuana katika mpambano huu.
Mwisho,
kutakuwa na resi za ngalawa zitakazofanyika tarehe 30 Julai, 2017, pia
katika fukwe za Vumawimbi Pemba.
Shindano litashirikisha ngalawa takribani 20
kutoka maeneo mbali mbali Kiswani Pemba kama vile Tumbe, Kiuyu, Msuka,
Shumba Mjini, Mwambe na Mnarani.
Tamasha hili limedhaminiwa na
ZURA (Zanzibar Utility Regulatory Authority) na litarushwa hewani na kituo cha Televisheni cha AZAM
ambao ni washirika wenza wa Kampuni ya Rafiki Network.
Kwa
niaba ya Rafiki Network, tunapenda kuwashukuru na kuwaomba watanzania wote kushiriki kwa njia moja
au nyengine katika kufanikisha tamasha hili.
Mwisho kabisa,
tunaomba na tunakaribisha vyombo vya habari kuja na kuripoti matukio haya ya kihistoria kwa maslahi ya maendeleo ya
Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
Ahsanteni,
Ali
Othman Ali
MkurugenziwaHabarinaMahusiano
RAFIKI NETWORK CO. LTD
No comments:
Post a Comment