Habari za Punde

Makamo wa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Azungumza na Balozi wa Israel Nchini Amaliza Muda Wake.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga  .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini anayemaliza muda wake  Mhe. Yahel Vilan.

Balozi huyo alikutana na Makamu wa Rais na kumuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia nchini ulikuwa umemalizika.
Makamu wa Rais alisema anafurahi kuona Idadi kubwa ya Watalii kutoka Israel wanaokuja Tanzania .

Tunawakaribisha sana Tanzania ,waje kwa wingi wao, tunawakaribisha kwa mikono miwili
na alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha  mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili.  
Kwa upande wake Balozi Yahel alisema watalii kutoka nchini Israel wameongezeka kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri , amani na utulivu wa nchi.
Balozi Yahel alisema atakuwa mjumbe wa kuitangaza Tanzania popote duniani .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.