Habari za Punde

Simba waanza kujifua Uwanja wa Amaan kujiandaa na mchezo wao wa ngao ya hisani na Yanga


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kikosi cha Simba jana Jumanne Agosti 15 kimeanza mazoezi yake katika uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar mazoezi ambayo yamefanyika kuanzia saa 3 za asubuhi katika uwanja huo.

Simba waliwasili Zanzibar jana Jumatatu wakitokea Jijini Dar es salam kwaajili ya kuweka kambi Mjini Unguja wakijiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga ambao nao jana asubuhi waliondoka Unguja na kwenda Pemba kwa ajili ya kambi pia.

Kambi ya Simba visiwani hapa watakaa mpaka Agosti 22, 2017 siku moja kabla ya mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Agost 23 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salam.

Abbas Suleiman ambae ni mratibu wa timu ya Simba amezungumzia sababu kubwa inayowavutia kuweka kambi Zanzibar ambapo amesema Zanzibar ni nyumbani kwao.

“Zanzibar ni nyumbani ndio mana tunapenda kuja kuweka kambi mara nyingi, na tunapenda kuja kuweka kambi hapa si tukikutana na Yanga tu hata baadhi ya mechi nyengine, hapana siri nyengine yoyote isipokuwa hapa ni nyumbani tu, kuna utulivu wa hali ya juu ndio mana tunapenda kuja Zanzibar”. Alisema Abbas.

Kambi ya Simba ipo kwenye Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.