Habari za Punde

Mahakama Yafuta Kesi ya Manji na Wezake ya Uhujumu Uchumi, Sasa Wapo Huru.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imewachia huru Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji na wenzake wawili waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi.

Manji na wenzake wameachiwa baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kuomba kuondolewa kwa mashitaka dhidi yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki.

Baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, kueleza nia hiyo ya DPP, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo aliliondoa na kuwaachia huru washitakiwa hao.

Manji na wenzake ambao waliletwa Mahakamani hapo wakitokea Mahabusu Gereza la Keko, waliondoka Mahakamani hapo kwa kutumia magari binafsi kurejea makwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.