Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Kilimani City na KMKM Uwanja wa Amaan Zanzibar KMKM Imeshinda Bao 3--0.

Mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City Ali Mohammed akimpita beki wa Timu ya KMKM Said Hamza wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya KMKM imeshinda bao 3-0. 
Mchezaji wa Timu ya KMKM Mudrik Muhibu akiokoa mpira golini kwao wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya KMKM imeshinda bao 3--0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Kilimani City Abdilah Seif Bausi akiwa katika jitihada za kutafuta bao wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya KMKM imeshinda Bao 3--0.

Benchi la ufundi la Timu ya Kilimani City wakitafakari kipigo cha bao 3-0 dhidi ya Timu ya KMKM katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar.
Kocha Mkuu wa Timu ya Kilimani City Ahmed Badru akiwa na mshangao baada timu yake kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Timu ya KMKM katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.