Habari za Punde

Wahariri wa Vyombo vya Habari Wapewa Taaluma Juu ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza akifunfungua warsha ya wahariri wa vyombo vya habari inayohusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Hoteli ya Golden Tulip Mlindi Mjini Zanzibar (kulia) Prof. Martin Mhando na kushoto Naibu Mkurugenzi Muendeshaji Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Said Bakar.
Naibu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dr. Juma Mohammed Salum akiwakaribisha wahariri wa vyombo vya habari katika warsha ya siku mbili ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi Muendeshaji Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Said Bakar akieleza utaratibu unaotumika katika zoezi la kutafuta mafuta na gesi asilia Zanzibar.
Mshauri wa usalama na afya  kwenye mafuta na gesi asilia  Respicious Kundama akiwasilisha mada ya mahusiano ya jamii juu ya athari za mazingira wakati shughuli hizo zikiendelea.
Mtaalamu wa utafutaji mafuta na gesi asilia kutoka kampuni ya Rakgas ya Rasil Khema Shari Hassan akielezea namna ya shughuli za utafutaji wa mafuta na gesiasilia utakavyofanyika kwa kutumia meli maalumu itakayowasili ijumaa ijayo.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo kutoka vyombo mbali mbali vya habari  wakifuatilia mada zinazotolewa.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo  Khatibu Suleiman akiuliza suala katika warsha hiyo inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.