Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AWASILI NAIROBI KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS UHURU KENYATTA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kenya Mhe. Robinson Githae na Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara Chana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni katika chumba cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.