Habari za Punde

Serikali Kutowafumbia Macho Wafanyabiashara wa Mbolea Wanaokwepa Bei Elekezi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Dkt Mary Mwanjelwa akizungumza katika Mkutano wa Makatibu Tawala na Washauri wa kilimo wa Mkoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Katika KUKUMBI WA kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya Nov 21 ,2017.

Na EmanuelMadafa,Mbeya

SERIKALI imewataka wafanyabiashara wa mbolea nchini kuhakikisha wanafuata bei elekezi ya uuzaji wa mbolea iliyowekwa na serikali ili kumsaidia mfanyabiashara mdogo aweze kuuza kwa rejareja.

Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Naibu waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa  wakati akifungua  mkutano wamakatibu Tawala na washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini .

Amesema kuwa endapo itagundulika kwamba kuna mfanyabiashara wa jumla anamuuzia mfanyabiashara wa rejareja kwa bei itakayomfanya ashindwe kuuza kwa bei elekezi wizara  itamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungia biashara yake

Mwanjelwa amesema ofisi yake inaushahidi kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wamekuwa wakiwauzia mawakala  wanaouza kwa bei elekezi ya serikali  hivyo kuleta mkanganyiko na kuwafanya wauze mbolea hiyo kwa bei zaidi ya elekezi .

Amesema katika Mikoa ya Ruvuma,Lindi ,Mtwara ,Mwanza na Geita wapo wafanyabiashara  ambao  sio waaminifu wamekuwa wakifungua  mifuko na kuuza mbolea ya kupandia  (DAP) kwa Shilingi 2,000 kwa kilo kwa lengo la kujipatia kiasi cha shilingi  laki moja (100,000) kwa mfuko wa kilo 50  badala ya bei elekezi ya shilingi  elfu hamisini na moja.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora wake kwa kufunguliwa kwa kuachwa wazi wafanyabiashara hao wanawaingizia hasara kubwa wakulima  hasa katika kipindi cha mavuno.

Kutokana hali hiyo Naibu waziri huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara  kote nchini kuacha tabia hiyo  mara moja ili kumpa fursa Wakala aweze kuuza kwa bei ya rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao .

Mkutano huo unalenga  kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu  mifumo mipya iliyoanzishwa  ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-BPS )na usimamizi wa mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata mbolea bora kwa bei  nafuu sanjali na kuongeza usalishaji wenye tija.

Mwisho.
Washiriki  wa Mkutano wa Makatibu Tawala Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaolenga  kuongeza uwezo uelewa wa pamoja kuhusu mifumo mipya iliyoanzishwa ya uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System -BPS) na Usimamizi wa bei ya mbolea ,katika ukumbu wa mikutano Mkapa jijini Mbeya Nov 21 mwaka huu.

Mshiriki akichangia katika Mkutano huo........

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa katika Piha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.