Habari za Punde

JUMIA KUWAWEZESHA WATANZANIA KUMILIKI SIMU ZA KISASA KWA BEI NAFUU Yapunguza bei za simu mpaka 60%! Mteja kuunganishwa na kifurushi cha internet ya bure kutoka Tigo mpaka GB 18

Na Jumia Tanzania
Katika kuhakikisha kwamba kila mtanzania anamiliki simu za kisasa na kwa bei nafuu, Jumia inaendesha kampeni ya ‘Mobile Week’ ambayo itadumu mpaka Machi 30. Tofauti na kampeni zake zingine kama vile ‘Black Friday’ ambayo huwa inajumuisha mauzo ya bidhaa tofauti, wiki hii ni maalum kwa ajili ya mauzo ya simu pekee kwa gharama nafuu, ukizingatia sikukuu ya Pasaka ikikaribia.

Jumia inaamini kwamba sekta ya simu ina mchango mkubwa katika maendeleo ya watanzania kwa upande wa kijamii na kiuchumi. Kwenye karne hii yenye maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, simu sio kifaa cha anasa tena kama ilivyokuwa awali bali ni nyenzo muhimu inayorahisisha maisha na shughuli za kila siku. Kwa mfano, hivi sasa simu hazitumiki tu kupata, kusambaza na kupashana habari bali pia hutumika kutuma na kupokea fedha, pamoja na kufanya malipo ya huduma mbalimbali kama vile umeme, maji, karo za shule, biashara, na hata uuzaji na manunuzi ya bidhaa.      


Akielezea umuhimu wa kampeni hiyo kwa wateja na sekta nzima ya mawasiliano ya simu nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott amesema kuwa maendeleo ya ukuaji wa kasi ya kiuchumi nchini yameifanya sekta hiyo kuwa ni muhimu na yenye mchango mkubwa kwa ukuaji wa sekta nyinginezo pia. 

“Hii ni kampeni ya kipekee kutokea nchini hususani katika mauzo ya bidhaa moja. Soko la simu limekuwa kubwa Tanzania likichochewa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa makampuni ya mitandao ya simu na yanayouza bidhaa hii. Changamoto kubwa ambayo Jumia tumeigundua na tungependa kuitafutia ufumbuzi ni upatikanaji wake kuwa wa ghali jambo ambalo si watanzania wote wanaweza kumudu. Lakini kupitia ‘Mobile Week’ wateja watajipatia simu za kisasa na mpya kabisa kwa bei iliyopunguzwa karibuni nusu yake. Bei ambayo ni nafuu na hauwezi kuipata hata ukienda kwenye maduka ya kawaida isipokuwa kwenye mtandao wetu pekee,” alifafanua Bw. Prescott.


“Lengo kuu la Jumia ni kubadili mtazamo na kujenga tabia ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao miongoni mwa watanzania wengi. Bado kuna idadi kubwa ya watanzania wanaamini kwamba manunuzi kwa njia ya mtandao sio salama. Tunataka kubadili dhana hiyo kwa sababu dunia ndipo ipo huko kwa sasa, ulimwengu wote umehamia kwenye mifumo ya mtandaoni. Kupitia njia hii wateja wataweza kuokoa muda na gharama ambazo wanaweza kuziwekeza katika shughuli zingine za kujenga taifa. Tunataka pia kubadili dhana kwamba kufanya manunuzi lazima iwe mwisho wa wiki. Kupitia mtandao wa Jumia sasa mtu yoyote anaweza kufanya manunuzi ya bidhaa anazozipenda na kuletewa mahali popote alipo bila ya kuathiri shughuli zake,” aliendelea kufafanua zaidi.

Katika ripoti iliyowasilishwa na Jumia siku za hivi karibuni ilibainisha kuwa watumiaji wa simu za mkononi pamoja na ueneaji wa mtandao wa intaneti inakuwa kwa kasi kubwa. Hivi sasa Tanzania, watumiaji wa simu za mkononi ni zaidi ya milioni 40, idadi ambayo ni sawa na asilimia 72 kwa ueneaji wake nchini. Kuongezeka kwa watumiaji hao kunaenda sambamba na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa intaneti ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya kuingia kwa simu za mkononi za kisasa. Watanzania wanaotumia intaneti kwa sasa wanafikia takribani milioni 23.      


Miongoni mwa sababu za ukuaji huo ni pamoja na uwepo wa ushindani wa bei sokoni hivyo kupelekea bei kuwa nafuu. Kwa kuongezea, maboresho na ofa zinazotolewa na kampuni za mitandao ya simu kama vile huduma za intaneti zimekuwa ni kichocheo kikubwa kwa watanzania kumiliki simu za mkononi.     

Akitoa wito kwa watanzania kuichangamkia ofa ya ‘Mobile Week,’ bosi wa kampuni hiyo inayojihusisha na manunuzi na uuzaji wa bidhaa mtandaoni, alihitimisha kwa kusema, “lengo la kampeni hii ni kuhakikisha kuwa watanzania wanaomiliki simu za mkononi wanaongezeka zaidi. Katika kulihakikisha hilo, tunawasihi wateja kuitumia wiki hii ipasavyo kwa sababu punguzo ni kubwa na kuna ofa kemkem kwenye mtandao wetu.”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.