Habari za Punde

Waziri Soud: Serikali inaongozwa kwa kufuata misingi ya katiba bila ya ubaguzi wowote


PEMBA / BAKAR MUSSA-ZANZIBARLEO.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, inayoongozwa na Rais wa Dkt, Ali Mohammed Shein, inaongozwa   bila ya ubaguzi wa aina yoyote na kwa kufuata misingi ya Katiba ya Zanzibar na inaendelea kuwaletea maendeleo Wananchi wake kwa kufuata ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

Akizungumza na Uongozi wa Serikali , Kamati ya Ulinzi na Usalama na masheha wa Mkoa wa Kusini Pemba Waziri asiekuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Said Soud Said, huko katika Ukumbi wa Baraza la Mji wa Chake Chake, alisema wale Viongozi wa Vyama vya Siasa wanaotumia majukwaa ya kisiasa  na kuwadanganya Wananchi kuwa Serikali ya Dkt, Shein, inaongozwa kwa misingi ya  ubaguzi  ni sawa na kekebehi  juhudi zinazochukuliwa na Rais wa  Zanzibar za kuwaletea maendeleo Wananchi .
Alieleza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , inayoongozwa na Dkt, Shein, chini ya chama Mapinduzi imekuwa ikitekeleza ahadi ilizozitowa katika Ilani ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015-2020 ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Unguja na Pemba katika Sekta zote muhimu za Kijamii bila ya kuangalia itikadi zao walizonazo.

Soud, aliwataka Masheha na Wananchi kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono na kumuamini  Dkt, Ali Mohammed Shein, juu ya Uongozi wake wenye hekima na busara zinazomuwezesha kuongoza Zanzibar kwa misingi ya Demokrasia.

“ Wale Viongozi wa Vyama vya Siasa wanaopita na kusema nchi hii , haina maendeleo kwa vile inaongozwa kwa misingi ya ubaguzi niwatu wasiokuwa na dira ya maendeleo na nikutafuta mtaji wa kisiasa kwani hakuna Mwananchi asieona maendeleo hayo kwa nyanja tafauti tafauti ,” alieleza.

Alifahamisha kuwa maendeleo yalioko Pemba katika kipindi cha utawala wa Dkt, Ali Mohamed Shein, ni ya kupigiwa mfano ambayo hayana ubaguzi , na hajawahi kuwepo hata katika awamu zilizopita na haya yamekuja baada ya kuwepo Amani na utulivu ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa upande wake , Waziri asiekuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanziba, Juma Ali Khatib, aliwaonya Viongozi wa Vyama vya Siasa kwa kutoyatumia majukwa ya kisiasa kwa kujijengea umaarufu huku wakiwa hadaa Wananchi Kisiwani Pemba , kwamba kutakuwa na mbadala wa Dkt, Shein na atatangwaza Kiongozi wa Upinzani.

Alisema hakuna mbadala wa Dkt, Ali Mohammed Shein, mpaka Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.

Alifahamisha kuwa wale Viongozi wa vyama vya Kisiasa wanaokaa wakiwahubiria Wananchi Siasa na kuwaacha wakitekeleza majukumu yao ya kujitafutia maendeleo kwani wakati wa kuhubiri mambo hayo ni mwaka 2020 na sio wakati huu.

“ Wananchi musikubali kugaiwa kwa misingi ya itikadi za Kisiasa bali , iungeni mkono Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , inayoongozwa na Dkt, Ali Mohammed Shein, kwani Serikali imetumia fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi yasiokuwa na shubha ya ubaguzi wowote,” alieleza.

Juma , alisema kuna baadhi ya Viongozi wamekuwa wakipita Kisiwani Pemba , na kuwadanganya Wananchi kuwa  ajira zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, zinatolewa kwa ubaguzi hayo ni upotoshaji kwani ajira za Serikali zinatolewa kwa uwazi na kutangazwa katika vyombo vya habari na kila mwenye sifa huomba na kupatiwa ajira kwa mujibu wa sifa zinazotakiwa na taasisi husika.

Hivyo aliwasihi Viongozi wa Vyama vya siasa kujaribu kuongoza Vyama vyao kwa kuiga hekma na busara za Dkt, Ali Mohammed Shein, na sio kutumia majukwaa ya kisiasa kwa kuwagawa Wananchi na kuichukia Serikali yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.