Habari za Punde

CCM kuwachukulia hatua watakaobainika kujihusisha na Rushwa katika Uchaguzi mdogo jimbo la Jang'ombeKatibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mjini Bi Fatma Juma Shomari amesema wamejipanga kuwachukulia hatua watakaobainika kujihusisha na Rushwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Jang'ombe unaotarajiwa kufanyika 27/10/2018 ili kupata kiongozi wenye sifa atakeweza kuongoza Jimbo hilo.
     Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari huko Afisini kwake Makadara Wilaya ya Mjini kuhusiana na uchukuaji wa Fomu kwa Upande wa chama cha Mapinduzi amesema kila inapofika kipindi cha Uchaguzi kuna madai ya kukijitokeza vitendo vya Rushwa hivyo wamejipanga kwa hali na mali kuhakikisha vitendo hivyo havitokei.
    Amesema cha cha Mapinduzi kiko mstari wa mbele kukemea Rushwa hivyo ameiomba Serikali kupitia vyombo husika kuungana katika kuwatia hatiani watakaobainika.
    Amefafanua kuwa kitendo cha kukamatwa watuhumiwa na kutofikishwa katika vyombo vya sheria kinapelekea kuwakatisha tamaa wananchi na kudumanza maendeleo ya nchi yetu.
     Ameeleza kuwa uzoefu unaonyesha kuwa kila ifikapo kipindi cha uchaguzi kumekuwa kukidaiwa kujitokeza baadhi ya watu wakijisshirikisha na vitendo hivyo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
     Ameeleza kuwa ili kukomesha suala hilo hakuna budi kutiwa hatiani kwa watakaobainika kutoa au kupokea Rushwa ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia ya kutenda tendo hilo.
     Aidha amewaomba Wanachama na Viongozi wa Jimbo la hilo kuendelea kuwa na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu kwani watapita watu wengi kudai kutaka kuchaguliwa kwa hali na mali na wengine hata kwa kuwa tayari kutoa Rushwa hivyo ni vyema kuepukana na watu hao.
    Mbali na hayo amewaomba Wanachama cha Mapinduzi jimbo la Jangombe wenye sifa  kujitokeza kwa wingi kuchukuwa fomu za kugombea kwa hiari bila kulazimishwa ili kutimiza haki yao ya Kidemokrasia ya kuchaguwa na kuchaguliwa.
    Hata hivyo amesema zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea Uwakilishi katika jimbo la Jangombe ndani ya chama chicho limeanza kutolewa tarehe 2/07/2018 hadi 3/07/2018,ambapo kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Jangombe unatarajiwa kufanyika tarehe 27/10/2018, kufuatia  aliekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Abdallah Maulid Diwani aliepoteza sifa za kuwa Mwakilishi wa jimbo.
              Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.