Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Viongozi Wakuu
mbalimbali wakiwemo, Marais Wastaafu, Makamu wa Rais Wastaafu, Mawaziri Wakuu
Wastaafu, Maspika Wastaafu na Majaji Wakuu Wastaafu wakati wa Kikao chake Ikulu
jijini Dar es Salaam.
. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na
Viongozi Wakuu mbalimbali wakiwemo, Marais Wastaafu, Makamu wa Rais Wastaafu,
Mawaziri Wakuu Wastaafu, Maspika Wastaafu na Majaji Wakuu Wastaafu mara baada
ya kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. Waliokaa mstari wa mbele ni Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi,(watatu kutoka kushoto), Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa(watatu kutoka kulia) Waziri Mkuu
Msaafu Cleopa David Msuya wapili kutoka kulia, Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani
Abeid Karume wapili kutoka kushoto, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika
wa Bunge Job Ndugai. Waliosimama mstari wa nyuma kutoka kulia kuja kushoto ni
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhan,
Spika Mstaafu Mama Anna Makinda, Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela, Waziri Mkuu
mstaafu Fredrick Sumaye, Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta, Spika wa Bunge
mstaafu Pius Msekwa, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowwasa, Makamu wa Rais Mstaafu
Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu
Msatafu Mizendo Pinda pamoja na Jaji
Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa
akizungumza katika mkutano huo Ikulu jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu
Edward Lowassa akizungumza katika mkutano huo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu John
Samwel Malecela akizungumza katika mkutano huo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza katika
mkutano huo Ikulu jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment