Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Akabidhi Zawadi Kwa Wanafunzi Waliopasi Michipuo Skuli ya Fuoni, Katika Sherehe ya Kuwaaga Iliofanyika Katika Viwanja Vya Skuli Hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita waliofanya vuzuri zaidi kwenye mitihani katika Sherehe ya kumaliza elimu msingi zilizofanyika katika skuli yao.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita waliofanya vuzuri zaidi kwenye mitihani katika Sherehe ya kumaliza elimu msingi zilizofanyika katika skuli yao.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi ya mashine ya kufulia, feni na Jiko Walimu wastaafu wa skuli ya Fuoni msingi, Asha Khamis na Hemedi  katika Sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza Darasa la sita  zilizofanyika Skulini kwao.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi zawadi ya mashine ya kufulia, feni na Jiko Walimu wastaafu wa skuli ya Fuoni msingi, Asha Khamis na Hemedi  katika Sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza Darasa la sita  zilizofanyika Skulini kwao.
Baadhi ya Walimu wa Skuli ya Fuoni msing wakionyesha furaha yao katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza masomo ya darasa la Sita yaliyofanyika katika Skuli yao.
Wanafunzi wa Skuli ya Fuoni msingi wakifuatilia Sherehe ya kuwaaga wanafunzi wenzao waliomaliza elimu ya msingi  katika sherehe zilizofanyika katika skuli yao.

Na Mwashungi Tahir            Maelezo       29-10-2018
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud  alisema maendeleo ya elimu  nchini yataendelea kuimarika  mwaka hadi mwaka  ili kufikia matarajio yaliyokusudiwa  katika muendelezo wa elimu.
Hayo aliyasema huko katika Skuli ya Fuoni ya msingi  A na B wakati alipokuwa akizungumza na walimu wazazi na wanafunzi kwenye uwanja wa skuli hizo katika sherehe ya kuwaaga na  kuwazawadia zawadi wanafunzi wa skuli hizo waliofaulu michipuo darasa la sita 2017  pamoja na walimu waliostaafu.
Alisema ushirikiano ni lazima kati ya walimu ,wazazi na wanafunzi katika kupatikana maendeleo na mafanikio ili yaweze kupatikana kama Serikali inavyokusudia  na kuweza kufikia kiwango kinachotakiwa juu ya elimu.
Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi baada ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964  imechukuwa juhudi ya kuweka elimu bure ili lengo wanafunzi wafaidike nayo kwa wenye uwezo na wasio na uwezo .
Aliwataka wanafunzi waliofaulu mchipuo kuingia kidato cha kwanza waongeze bidii wapasi vizuri katika kidato cha nne hadi kufikia cha sita na kuendelea na elimu ya juu zaidi  ili waweze kuwa wataalamu wazuri Serikalini.
“Jitahidini muendelee vizuri katika masomo yenu hadi kumaliza katika vyuo ili muweze kuwa wataalamu wazuri katika Serikali “.Alisema Mkuu huyo.
Pia aliushukuru uongozi unaotoa mafunzo  maalum ya kuwasaidia wanafunzi wanaofanya mtihani SSP Special Study Program  na kuwajengea uwezo  kuwaletea ufaulu watoto wengi kwa jitihada zao wanazozichukua  na faida zinaonekana.
Akitoa rai kwa walimu wa Skuli ya Fuoni msingi A na B kwa wale vijana wanaosoma mbali uongozi  SSP irudishe twisheni hapa skuli ya karibu badala ya kuifatia Kiembe samaki  kwa lengo la kupunguza gharama  kwa wazazi  na wao wanafunzi kwenda masafa marefu.
Hata hivyo alisema Serikali inafanya juhudi za kila mara katika kuongeza madarasa  na idadi ya walimu itaongezeka ili ifikie malengo yanayotarajiwa hapo baadae ya kupunguza idadi ya wanafunzi wengi katika madarasa.
Nae Mkuu wa Wilaya  ya Magharibi B Silima Haji wa Haji aliwahimiza walimu na wazazi pamoja na wanafunzi kuongeza mashirikiano katika kukuza elimu ili lengo linalotarajiwa liweze kufikiwa kwa ufaulu wa wanafunzi kwa wingi.
Pia aliupongeza uongozi wa program SSP kwa jitihada wanazozifanya na kufanikiwa kuweza kupasisha wanafunzi wengi  na kuwataka kuongeza bidii zaidi.
Jumla ya wanafunzi 42  wa Skuli za Fuoni msingi A na B na wamepata zawadi za uniform  sare za Skuli na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amewahidi kuwapa pesa za ushoni.
Kwa upande wa walimu waliostaafu Asha Khamis Suleiman ambaye alizawadiwa mashine ya kufuliya aliwataka walimu wawe na mashirikiano katika utendaji wao wa kazi  na kuwataka wajiepuswhe na majungu.
Pia aliwaomba waache kufanya kazi kwa mazowea  na wafuate miongozo ya kazi ili kwa lengo la kuifanikisha suala zima la ellimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.